Kwa miaka minne mfululizo Cristiano Ronaldo amekuwa katika orodha ya mwisho ya wachezaji bora wa UEFA ambao wamekuwa wakiwania tuzo ya Ulaya na mara hii pia yumo katika orodha hiyo akiwa pamoja na Arjen Robben na Manuel Neuer.
Mshambuliaji huyo wa Madrid Ronaldo atakuwa akitegemea kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuingia katika kinyang'anyiro hicho tangu kuanza kuteuliwa mwaka 2011 lakini akishindwa kutwaa tuzo hiyo katika kila igizo.
Mshindi huyo wa Ballon D'Or alikuwa na msimu mzuri uliopita akishinda tuzo ya Copa del Rey pamoja na taji la 10 kwa Madrid la michuano ya European Cup - La Decima.
Cristiano Ronaldo akifunga goli la rekodi la 17 katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya
Robben alishinda mataji mawili ya ligi na kikapu kwa Bayern Munich na alifunga na aliifungia magoli matatu Uholanzi katika kombe la dunia
Furaha: Manuel Neuer (katikati) alishinda Ligi na vikapu mara mbili akiwa na Bayern na kombe la dunia akiwa na UJerumani.
Hawa ni wale saba walioshindwa kutinga katika hatua ya mwisho
No comments:
Post a Comment