Pages

Saturday, August 23, 2014

CHELSEA 2 vs 0 LEICESTER CITY, DIEGO COSTA NA EDEN HAZARD WAIPA USHINDI BLUES DARAJANI!

Diego Costa akishangilia bao lake huku bao jingine likifungwa na Eden Hazard
Diego Costa akishangilia baada ya kuifungia bao Chelsea.
Bao mbili za Kipindi cha Pili za Diego Costa na Eden Hazard zimewapa Chelsea ushindi wao wa pili mfululizo kwenye Msimu mpya wa Ligi Kuu England dhidi ya Timu zilizopanda Daraja Msimu huu kwa Leo hii kuichapa Leicester City Bao 2-0 Uwanjani Stamford Bridge.
Wiki iliyopita waliipiga Bao 3-1 Burnley.
Diego Costa aliipa Bao Chelsea katika Dakika ya 63 alipounganisha krosi ya Branislav Ivanovic na hilo ni Bao lake la pili katika Mechi mbili za Ligi.
Bao la Eden Hazard lilifungwa Dakika ya 77 baada ya Shuti lake kumbabatiza Beki wa Leicester Wes Morgan na kumhadaa Kipa Kasper Schmeichel.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Agosti 23

Aston Villa 0 vs 0 Newcastle
Chelsea 2 vs  0 Leicester
Crystal Palace 1 vs West Ham
Southampton 0 vs 0 West Brom
Swansea 1vs 0 Burnley

No comments:

Post a Comment