Pages

Friday, August 1, 2014

BREAKING NEWSSSSSSSSSS!! KIFAA KIPYA CHA SIMBA CHAWASILI MCHANA HUU

Pierre Kwizera akiwasili leo



KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Pierre Kwizera anamewasili nchini leo akiwa na matumaini kibao ya kuisaidia Simba katika msimu ujao.
Kwizera ambaye amewasili majira ya saa nane na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya kesho atasaini Mkataba wa kuichezea Simba katika msimu ujao.
Kiungo huyo anayechezea klabu ya Afad Abidjan ya Ivory Coast amesema matarajio yake ni kusaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na hatimaye kuwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa .
“Naijua Simba ni timu kubwa lakini kwa hivi karibu haijawezza kushiriki mashindano ya kimataifa hivyo nitacheza kuhakikisha timu inafanya vizuri ili kukata kiu ya mashabiki”, alisema Kwizera
Mchezaji huyo atakuwa wanne kwa wachezaji wa kigeni huku akisubiriwa Paul Kiongera kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba ni mabeki Mkenya Donald Mosoti, Mganda Joseph Owino na mshambuliaji Amisi Tambwe wa Burundi.

No comments:

Post a Comment