Pages

Thursday, July 17, 2014

VAN GAAL AKIWA KATIKA SIKU YAKE YA KWANZA KABISA YA MAZOEZI YA MANCHESTER UNITED, IFAHAMU RATIBA NZIMA YA MICHEZO YA MAANDALIZI NCHINI MAREKANI


Louis Van Gaal (Video juu) akiwa katika siku ya kwanza ya mazoezi na wachezaji wake wa Manchester United.
Meneja huyo mpya aliyepewa jina la utani 'Iron Tulip' alionekana akizunguka uwanja wa mazoezi na kujumuika na wachezaji wake kwa mara ya kwanza sambamba na mchezaji mpya aliyesajiliwa msimu wa huu wa uhamisho wa kiangazi kwa ada ya uhamisho ya pauni £28 Ander Herrera.

Hii leo anatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari Old Trafford saa tisa mchana,  kabla ya hapo kesho kuelekea nchini Marekani  kwa maandalizi ya kikosi kuelekea kwenye msimu mpya.
Ikiwa nchini Marekani, United itacheza dhidi ya Los Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na Real Madrid, wakati ambapo mchezo wake wa kwanza kwa Van Gaal baada ya kutua Old Trafford ukiwa wa kirafiki dhidi ya Valencia Agosti 12.
Siku nne baadaye United itafungua msimu kwa mchezo wa kwanza wa ligi ya Barclays Premier League uwanja wa Old Trafford dhidi ya Swansea.

No comments:

Post a Comment