Pages

Friday, July 18, 2014

Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wanasema mchezi dhidi ya Msumbuji utakuwa mgumu wanahitaji zaidi sala na dua za Watanzania


Mshambuliaji wa Stars Thomas Ulimwengu
 Washambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samata pamoja na Thomas ulimwengu wamewataka watanzania kuwa kitu kimoja katika kipindi hiki ambapo timu yao ya taifa 'Taifa Stars' inakabiliwa na mchezo muhimu wa kuwani kufuzu kucheza fainali za Afrika za mwaka 2015 dhidi ya timu ya taifa ya Msumbiji.
Washambuliaji hao wawili wamesema hayo mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam tayari kwa kujiunga na wenzao katika maandalizi ya mwisho ya kuelekea katika mchezo dhidi ya Msumbiji ambao utachezwa mwishoni mwa juma hili mwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Theomas Ulimwegu wamesema mchezo huo utakua mgumu kutokana na kila upande kuhitaji kusonga mbele kwenye hatua ya makundi, hivyo hakuna njia ya mkato zaidi ya wachezaji kufanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wanashinda mchezo huo.
Kwa upande wa Mbwana Samata amesema maandalizi waliyoyafanya wakiwa na kikosi cha TP Mazembe kilichoweka kambi nchini Tunisia kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya klabu bingwa barani Afrika, yanatosha kwenda sambamba na wachezaji wa Stars ambao kwa kipindi kirefu walikua kambini chini ya kocha kutoka nchini Uholanzi Mart Nooij.
Samata amesema pamoja na kutabiri mchezo mgumu kati ya Tanzania dhidi ya Msumbiji bado anaamini viwango vya timu zote mbili vinashabihiana.
Katika hatua nyingine timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) itawasili jijini Dar es Salaam kesho tayari kwa mpambano wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika za mwaka 2015 dhidi ya Taifa Stars.
The Mambas watatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa 7.30 mchana kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na Jeffrey Constatino.

Wengine ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na Zainadine Junior.

No comments:

Post a Comment