Pages

Wednesday, July 30, 2014

Origi akamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Liverpool

 

Divock Origi hatimaye akamilisha uhamisho wa kujiunga na Liverpool
Hatimaye Liverpool imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Belgium Divock Origi akitokea klabu ya Lille ya Ufaransa kwa kitita cha pauni milioni £10. 

Origi atasalia Lille mpaka 2015
Origi mwenye umri wa miaka 19 kimsingi amekubali kuingia kandarasi ya miaka mitano lakini ataendelea kusalia katika klabu yake hiyo kwa mkopo msimu ujao huku akitarajiwa Anfield mwakani 2015.
"Ninafuraha na kujisikia fahari kujiunga na klabu kubwa kama Liverpool nimefurahi sana"
Origi alicheza michezo yote mitano ya Belgium katika kombe la dunia la FIFA 2014 kuelekea robo fainali na laifanikiwa kufunga goli katika mchezo dhidi ya Urusi
Wachezaji waliosajiliwa na Liverpool uhamisho huu wa kiangazi ni hawa wafuatao
Mshambuliaji Rickie Lambert miaka 32, amesaini kwa pauni milioni £4 akitokea Southampton


Kiungo Adam Lallana miaka 25, amesaini kwa pauni milioni £25 akitokea pia Southampton
Kiungo Emre Can, miaka 20, amesaini kwa pauni milioni £10 akitokea Bayer Leverkusen
Winga Lazar Markovic, miaka 20, amesaini kwa pauni milioni £20 akitokea Benfica
Mlinzi Dejan Lovren, miaka 25, amesaini kwa pauni milioni £20 Southampton
Na sasa mshambuliaji kinda Divock Origi, mwenye umri wa miaka 19 amesaini kwa pauni milioni £10 akitokea Lille
Origi alianza soka lake katika klabu ya Genk kabla ya kuelekea Lille akiwa ana umri wa miaka 15.

No comments:

Post a Comment