Pages

Tuesday, July 22, 2014

MARIO BALOTELLI AWACHANA LIVE ARSENAL KUHUSU POSHO YAKE YA MWAKA


 Balotelli akiwa na mpenzi wake Fanny Neguesha walipokuwa katika duka la vifaa vya michezo la Puma
Balotelli anatarajiwa kuelekea katika klabu yake ya AC Milan kwa maandalizi ya msimu nchini Marekani
Mario Balotelli anataka pauni milioni £5 kwa mwaka nje ya makato ya kodi kama Arsenal wanataka ajiunge nao msimu wa usajili wa kiangazi.
The Gunners wameonyesha nia kwa mshambuliaji huyu wa kimataifa wa Italia baada ya kuwepo fununu kuwa klabu yake ya AC Milan iko tayari kumuuza.
Arsenal ni kama wameingiwa na baridi ya kuendelea na Balotelli kufuatia kuwepo na maendeleo mazuri katika mpango wao wa kumsajili Loic Remy lakini pia inaonekana mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Queens Park Rangers unaonekana kukwama kutokana na mshahara anao hitaji mshambuliaji huyo.
Kwasasa washika mitutu ni kama wameanza tena kuamsha mpango wa  Balotelli lakini pia na hilo linakumbwa na kigagaziko kutokana na mshahara mkubwa unaotakiwa na Balotelli.
Klabu hiyo ya London ya kaskazini imekaririwa ikisema kuwa wana uwezo wa kumlipa kwa wiki pauni £100,000.
Winner: Balotelli celebrates scoring against England for Italy during the World Cup group stages
Balotelli akishangilia goli aliloifungia Italia dhidi ya England katika fainali za kombe la dunia hatua ya makundi
Him again: Former Man City star Balotelli (left) has been linked with a move to Arsenal
Nyota wa zamani wa Man City Balotelli (kushoto) amekuwa akihusishwa na kujiunga na Arsenal
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City yuko Marekani akiwa na mpenzi wake Fanny Neguesha, akimalizia mapumziko yake ya baada ya fainali ya kombe la dunia.
Having fun: Balotelli uploaded a picture of him and girlfriend Fanny Neguesha outside Empire State Building
Balotelli akitupia picha akiwa na mpenzi wake Neguesha nje ya jengo la Empire.

No comments:

Post a Comment