Pages

Thursday, July 24, 2014

Malkia azindua michezo ya madola


Malkia Elizabeth ameifungua rasmi michezo hiyo kwa kuusoma ujumbe wake uliokuwa umehifadhiwa katika kile kinachofahamika kama the Commonwealth baton yaani mwenge wa jumuiya ya madola.
Maelfu ya wanamichezo kutoka nchi 71 wameshiriki katika ufunguzi huo mbele ya watu elfu 40 waliokuwa uwanjani huku dunia ikifuatilia kupitia vyombo vya habari.
Hali ya hewa katika mji wa Glasgow leo imetambulishwa rasmi kuwa ndiyo yenye joto Zaidi kwa mwaka huu baada ya kufikia digrii 25c.
Michezo hiyo itahusisha michezo 17 kwa siku 11.
Michezo ya jumuiya ya madola uhusisha nchi zilizowahi kuwa chini ya utawala wa himaya ya uingereza.

No comments:

Post a Comment