Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu |
Uongozi
wa klabu Simba umemuongezea mwaka mmoja kocha mkuu wa klabu hiyo
Zdravko Logarusic baada ya kuhitimisha mkataba wa awali nusu mwaka.
Akiongea
hii leo katika makao makuu ya klabu hiyo, makamu mwenyekiti wa klabu ya
Simba Geofrey Nyange Kaburu amesema uongozi wa Simba umeridhishwa na
kocha Logarusic na kwamba kuanzia sasa atakuwa akisimamia timu zote ya
wakubwa na vijana akisaidiana na kiungo za zamani wa klabu hiyo Selemani
Matola.
Kaburu
amesema ndani ya mkataba mpya na Loga kunaweza kukafanyika mabadiliko
ya ama kumfuta kazi au kumuongezea muda zaidi kutegemeana na makubaliano
ya kimsingi ambayo ni pamoja na uwezo wa kiuchezaji wa kikosi cha
Simba.
Kocha Loga wa Simba. |
Kaburu
amesema wanaamini kuwa kocha huyo atairejesha klabu yao katika heshima
yake kama ilivyokuwa huko nyuma, ambapo Simba kama itakumbukwa ilimaliza
katika nafasi ya nne katika msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Kwa
upande wake kocha Loga ameahidi kufanya mazuri kubadilisha soka na
matokeo ya Simba kwani ni klabu kubwa ambayo ina mashabiki wengi ambao
wana presha kubwa nyuma yake.
No comments:
Post a Comment