Mlinda
mlango Husein Sharif maarufu kama Casillas (Pichani juu akiwa na Kocha
wa makipa wa Taifa Stars Juma Pondamali) amejiunga na klabu ya Simba kwa
mkataba wa miaka miwili akitokea kwa wakata miwa wa Mtibwa Sugar ya
Morogoro. Mlinda mlango huyo ambaye alikuwa ngome kubwa ya milingoti
mitatu ya watoto wa Manungu Turiani , amekwenda kuchukua nafasi iliyo
achwa wazi na mlinda mlango raia wa Ghana Yaw Berko aliyemaliza mkataba
wake na wekundu hao wa Msimbazi. Taarifa za kukamilika kwa usajili wa
mlinda mlango huyo pamoja na wachezaji wengine wawili vijana Manyika
Opeter na Ibrahim Hajibu zimethibitishwa na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu mchana wa leo. |
No comments:
Post a Comment