KLABU ya Galatasaray ya
Uturuki, imethibitisha kuwa wameanza mazungumzo na kocha wa zamani wa
Italia Cesare Prandelli.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 aliachia
nafasi yake kama kocha wa timu ya taifa ya Italia baada ya kuenguliwa
katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia kwa kupokea vipigo kutoka kwa
Uruguay na Costa Rica.
Galatasaray imekuwa katika mawindo ya muda mrefu
ya kutafuta kocha mpya kufuatia kuondoka kwa Roberto Mancini baada ya
timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili katika msimo wa Ligi Kuu nchini
humo.
Katika taarifa ya klabu hiyo iliyotumwa katika mtandao imedai
kuwa wameanza mazungumzo na mashabiki watajulishwa kuhusu maendeleo ya
mazungumzo hayo.
Galatasaray inatarajiwa kushiriki michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya Fenerbahce kufungiwa kushiriki
michuano yote ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment