Pages

Thursday, July 24, 2014

BECKHAM AITEMBELEA MANCHESTER UNITED LA GALAXY

WAKATI himaya mpya ya Meneja mpya Louis van Gaal imeanza Jumatano huko Pasadena Rose Bowl kwa Washabiki 70,000 kufurika kuiona Manchester United, Mchezaji wa zamani wa Timu hizo mbili David Beckham alitembelea Hoteli ya Beverly Hills kuwasabahi Marafiki zake wa Man United.
Beckham, Lejendari wa Man United, yuko huko Los Angeles kwa matembezi na alifika Hotelini na kuongea na Wachezaji wa Man United na Mameneja wao, Louis van Gaal na Ryan Giggs, ambae waliwahi kucheza pamoja huko Man United tangu wakiwa wadogo.
Ingawa Mechi hii ni ya Kirafiki, Mshindi hutunzwa Chevrolet Cup, Mashabiki wa Man United walifuatilia kwa hamu kuona Van Gaal anaanza vipi wadhifa wake.

Wiki nzima kwenye Mazoezi Man United wamekuwa wakitumia Mfumo wa 4-3-3 na  wameutumia kwenye Mechi na LA Galaxy.
Lakini pia mvuto ni kuwaona Wachezaji wapya, Ander Herrera na Luke Shaw, wakivaa jezi ya Man United kwa mara ya kwanza.
Mmoja wa Wachezaji wa LA Galaxy ambae Man United watamjua vizuri ni Mchezaji wa zamani wa Tottenham na Liverpool ambae sasa ni Nahodha wa Republic of Ireland, Robbie Keane.
Baada ya Mechi hii, Man United watasafiri kwenda Miji ya Denver, Washington na Detroit kucheza na AS Roma, Inter Milan na Real Madrid kwenye Mashindano ya International Champions Cup.

No comments:

Post a Comment