Pages

Friday, July 11, 2014

ARSENE WENGER: KUTUA KWA ALEXIS SÁNCHEZ NI KUVUNA MAKOMBE TU

Arsenal imethibitisha kumsaini Fowadi wa Chile anaechezea Barcelona Alexis Sanchez kwa Dau linalokadiriwa kuwa Pauni Milioni 30.
Sanchez, mwenye Miaka 25, amesaini Mkataba wa muda mrefu unaosadikiwa kuwa wa Miaka Mitano baada kufuzu upimwaji Afya yake uliofanyika Leo Jijini London kwenye Kituo cha Mazoezi cha Arsenal cha Colney.

Mchezaji huyo wa Chile aling’ara huko Brazil kwenye Kombe la Dunia na Nchi yake ilitolewa na Wenyeji Brazil kwa Penati katika Raundi ya Pili. 
Awali iliaminika Sanchez atakwenda Liverpool kwenye Dili inayomhusisha Luis Suarez kuihama Liverpool na kwenda Barcelona lakini Mchezaji huyo aliamua angependa kujiunga na Arsenal.
Sanchez amedumu Barcelona kwa Misimu Mitatu baada kuhamia kutoka Udinese ya Italy na kufunga Bao 39 huko Spain.
Akimkaribisha huko Emirates, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema Mchezaji huyo ataongeza nguvu, ubunifu na ubora katika azma yao ya kutwaa Ubingwa ambao wameukosa kwa zaidi ya Miaka 10 sasa.

Sanchez anakuwa Mchezaji wa pili alienunuliwa na Arsenal kwa Bei mbaya kufuatia Mesut Ozil Msimu uliopita.
Arsenal wanatarajiwa pia kumnasa Beki wa France anaecheza Newcastle, Mathieu Debuchy, kwa Dau la Pauni Milioni 11 huku Wenger akiwawinda Loic Remy wa QPR na Kiungo wa Germany Lars Bender.
Ni raha kuwa mahala hapa! Nitafanya lolote timu yangu ya sasa Arsenal kuleta mabadiliko na kuendeea kunyakua vikombe!

No comments:

Post a Comment