GOLIKIPA wa timu ya taifa ya Algeria, Rais M’Bolhi amesisitiza kuwa kipigo cha mabao 2-1 walichpata kutoka kwa Ujerumani katika muda nyongeza hakuhisiani na wachezaji wenzake kuwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Golikipa huyo ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo kutokana na kuokoa michomo mingi sana ya Ujerumani katika muda wa kawaida kabla ya Andre Schurrle na Mesut Ozil hawajafunga mabao katika muda wa nyongeza na kuifanya Algeria kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo M’Bolhi amesema hadhani kama wachezaji kuwepo katika mfungo kulichangia wao kufungwa katika mchezo huo kwani walijiandaa kucheza kwa muda wowote ambao ungehitajika. M’Bolhi aliendelea kudai kuwa hakuna mtu yoyote ambaye aliamini kwamba wanaweza kucheza vyema kama walivyofanya ni bahati mbaya iliyowakuta na kuwafanya wakubali kufungwa mabao mawili katika muda wa nyongeza.
No comments:
Post a Comment