Pages

Sunday, June 29, 2014

WORLD CUP: BRAZIL 1 vs CHILE 1, WENYEJI BRAZIL WAPETA!! WASHINDA KWA MIKWAJU YA PENATI 3-2! KIPA JULIO CESAR AIOKOA!

Wachezaji wa Brazil wakimpongeza kipa wao baada ya kuimili mikikimikiki ya Mishuti langoni leo hii huko Mineirao Stadium - Belo Horizonte Nchini Brazil ambapo Fainali hizi zinafanyikia.BKwenye Mikwaju ya Penati wenyeji Brazil wameifunga timu ya Chile bao 3-2, Baada ya Mtanange kumalizika 1-1 na kwenda hatua ya pili ya dakika 120. 
WENYEJI Brazil na Chile zilikwenda Dakika 120 huko Estádio Governador Magalhães Pinto, Jijini Belo Horizonte, kwenye Mechi ya Raundi ya Pili ya Fainali za Kombe la Dunia baada kutoka Sare 1-1 katika Dakika 90 na pia kumalizika hiyo nyongeza ya Dakika 30 bila Mshindi na hatimae Brazil kupita kwa Mikwaju ya Penati 3-2 huku Kipa wao Julio Cesar akiibuka Shujaa kwa kuokoa Penati 2 kati ya hizo.Hulk reacts after a decision doesn't go his way
Brazil walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 18 la David Luiz alieunganisha Mpira uliopigwa Kona na Neymar na kugongwa na Thiago Silva.

Chile walisawazisha kwenye Dakika ya 32 kwa Bao la Alexis Sanchez.
Kipindi cha Pili Hulk aliifungia Brazil Bao la Pili lakini Msaidizi wa Refa Howard Webb kutoka England aliashiria Mbrazil huyo alishika kabla kufunga.

Hadi Dakika 90 kumalizika Bao zilikuwa 1-1 na Nyongeza ya Dakika 30 haikuzaa Mshindi na Mechi kuingia Tombola ya Mikwaju ya Penati ambazo Brazil walishinda kwa Penati 3-2 na kutinga Robo Fainali ambapo watakutana na Mshindi kati ya Colombia na Uruguay wanaocheza baadae leo.
Mtanange ulimalizika kwa sare ya 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika 90 na wakalazimika kwenda kucheza dakika 120, Ambapo na dakika hizo zilimalizika kwa 0-0(1-1) na kwenda katika Mikwaju ya penati.Kidogo tuandike 2-1!! Jamaa alisaidiwa na mkono Hulk na Mwamuzi kumuona na kusema hakuna!!

Alexis Sanchez akishangilia bao alke la kusawazisha katika dakika ya 32Alexis Sanchez of Chile celebrates scoring his team's first goal with teammates1-1, wachezaji wakipongezana!A general view of the stadiumTaswira
1-1Alexis Sanchez akishangilia bao lake la kusawazisha 1-1 katika kipindi cha kwanza, Ambapo timu zote mbili zimeenda kupumzika zikiwa sare ya bao 1-1.
Mchezaji anayekipiga katika Klabu ya Barcelona Alexis Sanchez ndie aliyewasawazishia bao Chile na kufanya 1-1 dhidi ya Brazil katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza.

Bao...David Luis akipumua baada ya kufunga bao

Mashabiki wa ChileShabiki wa Brazil akiwaombea wasonge mbele tuu!!!

Thiago Silva na mchezaji wa  Chile  Mauricio Pinilla wakiombana yaishe na kutakiana heri kipute kiendelee baada ya kukwatuana chini. wakikubaliana kwamba majambo kama yapo ya kawaida kwenye soka!!
Wachezaji wa Brazil wakipongezana walipopata bao lao kwenye dakika za kipindi cha kwanza.Mpaka ndani ya nyavu............David Luiz akitoa onyo!! ...sote ni wachezaji tucheze !Kipa Julio Cesar akiokoaMapumziko!MapumzikoBrazil take on Chile in the last 16VIKOSI:
Brazil: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Fernandinho, Gustavo, Hulk, Oscar, Neymar, Fred.
Subs: Jefferson, Paulinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Maicon, Victor.

Chile: Bravo, Mena, Isla, Silva, Alexis, Vidal, Vargas, Medel, Jara, Aranguiz, Diaz.
Subs: Toselli, Albornoz, Carmona, Pinilla, Valdivia, Rojas, Orellana, Beausejour, Gutierrez, Fuenzalida, Paredes, Herrera.

Referee: Howard Webb (England)


No comments:

Post a Comment