Usiku huu pia, Kocha wa Real, Carlo Ancelotti, ameweka Historia ya kutwaa Taji la 3 Ulaya kama Meneja na kuifikia Rekodi ya Meneja wa Liverpool, Bob Paisley, ambae pia ametwaa Mataji Matatu.
Lakini kama si ushujaa wa Sergio Ramos, ndoto hii ya Real isingetimia kwani walikuwa wameshakufa Bao 1-0, Dakika 90 zilimalizika, na kwenye Dakika ya 3 ya Dakika 5 za Nyongeza, Ramos ndie alieisawazishia Real.
Fainali hii ilipoanza, kwenye Dakika za mwanzoni, Real ndio walionyesha wako juu na Atletico kupata pigo Dakika ya 9 tu baada ya Straika wao mahiri, Diego Costa, kulazimika kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Lopez.
Hata hivyo, Atletico walionekana kuikamia sana Mechi hii na kutowapa nafasi Real kutuliza Mpira kiasi ambacho nafasi pekee kwa Real katika Kipindi cha Kwanza ilikuwa ni ya Gareth Bale ambae alipiga nje akiwa kwenye nafasi nzuri sana kufunga na mara baadae Real wakatoa Kona ya kipuuzi ambayo ilileta madhara makubwa kwao.
Makosa makubwa ya Kipa Nambari Wani wa Spain, Iker Casillas, ndio yaliowapa Atletico Bao lao katika Dakika ya 36 baada kupigwa Kona na kuokolewa na Mpira kumkuta Diego Godin, Mchezaji kutoka Uruguay, aliepiga Kichwa kuurudisha Mpira Golini lakini wakati huo Casillas alikuwa keshatoka Golini na Kichwa hicho kumpita juu na licha ya juhudi zake kurudi mstarini na kuokoa hakufanikiwa.
Diego Godin ndie aliewapa Atletico Ubingwa La Liga Wikiendi iliyopita baada Kichwa chake kuipa Bao la kusawazisha huko Nou Camp walipotoka 1-1 na Barcelona na Bao la Leo kwa Atletico ni Bao lake la 8 Msimu huu – na yote ni Kichwa.![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_uZlmQTM60Ov0w7JxoccCH2NCFNcx1zoxXIg6LN_jQIuFVx_ZfxYCH5Na_EcxYkgLQTOD_tSHg2OPGFGs752GA1AkJONU2nh9VclsTaNu1ruaEZB2S1dyqFnrigTZlf-XglKW8Yqpj3gBy15pTSE0tZHoiHsBo9nBM5xSP_Wq0WjO0HSOeUzn5aHg=s0-d)
Hadi Mapumziko Atletico walikuwa mbele kwa Bao 1-0.
Kipindi cha Pili Atletico walianza vyema lakini kadiri Dakika zikiendelea kuyoyoma Real ndio walikuja juu na hasa Dakika 20 za mwisho lakini umaliziaji mbovu, hasa Bale, na Difensi ngangali ya Atletico iliwazuia.![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_uW2H2nUckNThksJkK8ohnjCzOsB1-Q3YhYLoCy4RjNssAXo6RvpVDalTSkLzCLOnxweux0mj4E1WaHD5O1GjCbvRCSsEX9H9tdMH6xlkfVCxwlocJ-znLH32G3NBO7obPPHp3WuRWrQGyUCLGhN7Fpn8NyjFxsM682hhuazk8b8EN2mN5SCJIa=s0-d)
Kipindi cha Pili Atletico walianza vyema lakini kadiri Dakika zikiendelea kuyoyoma Real ndio walikuja juu na hasa Dakika 20 za mwisho lakini umaliziaji mbovu, hasa Bale, na Difensi ngangali ya Atletico iliwazuia.
Baada Dakika 90 kumalizika na Bango kuashiria Dakika 5 za Nyongeza, kwenye Dakika ya 93, Kona ya Real iliunganishwa kwa Kichwa safi cha Sergio Ramos na kuipa Real Bao la kusawazisha na Mechi kwenda Dakika 30 za Nyongeza.![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vRoAtjLfwTREgyta63nElLQ8Xdd0AlsqOaRSNrE907-_7TCp7q12s0Z9p7HHHUhn70haIxUF2ASCga_-CWMHBj2yCH9cnXRG63fMJdTlXr3lfDQ-pIllFdzQfDWpFUwvVPbV6Dpe-4qx5c4PZlDrnc0YIrVlbtCnDhSbDlMyGhzklT_XzUibzCwQ=s0-d)
Hilo lilikuwa Bao la 6 kwa Ramos katika Mechi 7 zilizopita.
Nusu ya Kwanza ya Dakika za Nyongeza 30 haikuzaa Bao lolote.
Dakika ya 110, Angel Di Maria alikata mbuga toka kushoto na Shuti lake kuokolewa na Kipa Courtois na kumkuta Gareth Bale aliefunga kwa Kichwa na kuipa Real uongozi wa Bao 2-1.
Dakika ya 117 Pasi ya Ronaldo ilimkuta Marcelo ambae alisonga mbele na kuachi Shuti la chini na Real kupiga Bao lao la 3.
Nusu ya Kwanza ya Dakika za Nyongeza 30 haikuzaa Bao lolote.
Dakika ya 110, Angel Di Maria alikata mbuga toka kushoto na Shuti lake kuokolewa na Kipa Courtois na kumkuta Gareth Bale aliefunga kwa Kichwa na kuipa Real uongozi wa Bao 2-1.
Dakika ya 117 Pasi ya Ronaldo ilimkuta Marcelo ambae alisonga mbele na kuachi Shuti la chini na Real kupiga Bao lao la 3.
Dakika ya 119, Ronaldo alifunga Bao la 4 kwa Penati baada ya yeye mwenyewe kuchezewa Rafu na Godin.
Hilo ni Bao la 17 kwa Ronaldo kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu hu…NI REKODI MPYA.
Hilo ni Bao la 17 kwa Ronaldo kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu hu…NI REKODI MPYA.
Hadi mwisho Real 4 Atletico 1, NDOTO YA ‘LA DECIMA’ IMETIMIA!
Basi la Atletico Madrid
Basi la Real Madrid
Figo akijikosha kwa kubeba kombe la UEFA huku akiwatamanisha washikaji wa Mji mmoja
Mipango ilianzia hapa........
Atletico nao walianzia mizuka hapa
Hakunaga maandalizi kama haya!!
Kikosi cha Atletico kilichoanza
Kikosi cha Real Madrid
Dakika 8 mtu alitoka uwanjani ...Costa
Ronaldo akijisikilizia kwa kulalamika baada ya kufanyiwa majanga
Kwa Timu hizi haya kukosekana ni kazi pevu!!
Kocha wa Atletico Simeone
Kocha wa Real Madrid Ancelotti
Ronaldo akipiga frii kiki
Nini tena Ronaldo??
Ronaldo akifanya vitu vyake..
Ramos akiwasikilizia mashabiki wake baada ya kugeuza usiku kuwa mchana Lisbon
Marcelo akikumbatiana na kipa wake
Bale akiwafanya Atletico Madrid
Ronaldo alifunga mkwaju wa penati..
Nipishe!! Ronaldo akishangilia ao lake la penati
Sintofahamu zilifuatia!!
Tupe chetu!!!
No comments:
Post a Comment