Timu zikiingia uwanjani.
Wachezaji wakisalimiana
Kikosi cha Kagera kilichoanza
Waamuzi wa Mtanange huu kati ya Kagera Sugar na Simba
Benchi la Simba
Mchezo umemalizika Kaitaba ambapo wenyeji wa uwanja huo wamewakaribisha wekundu wa Msimbazi Simba sc.
Mtanange umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Simba walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa Zahor Idd Pazzi akipokea krosi kutoka kwa nahodha wao, Nassor Masoud Cholo.
Kagera walisawazisha bao hilo dakika ya 51 kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wao hatari, Them Felix `Mnyama`.
Kwa matokeo hayo, Simba sc wamefikisha pointi 37 katika nafasi ya 4 baada ya kushuka dimbani mara 24.
Kagera Sugar wamefikisha pointi 34 katika nafasi ya 5 baada ya kushuka dimbani mara 23.
Mechi ya Kaitaba haikuwa na ushindani mkubwa kwani timu zote hazikuwa na cha kupoteza, kwa maana ya kutotafuta ubingwa wala nafasi ya pili.
Timu zote zilikuwa zinashambuliana kwa zamu, lakini Kagera Sugar walipata nafasi nyingi zaidi ya Simba.
Hata hivyo ubutu wa safu za ushambuliaji kwa timu zote, kumeamuru matokeo yawe 1-1 mpaka dakika 90 zinamalizika.
Mashabiki wa Timu ya Simba SC Kaitaba wakiipa nguvu timu yao kwa kushangilia..
Mashabiki wa Simba
Azam Tv, Picha zikichuliwa live juu ya paa za jukwaa kuu kwenye Uwanja wa Kaitaba leo hii wakati wa kipute kilichomalizika kwa bao 1-1
Wadau..
Hapa hukatizi..
Wachezaji wa Kagera Sugar wakipongezana baada ya kusawazisha bao na kufanya 1-1 dakika ya 48
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakishangilia...
Furaha za hapa na pale za mashabiki wa Kagera baada ya timu yao kusawazisha bao
Mashabiki wa Kagera Sugar
Kipute kikiendelea
Mchezaji wa Kagera aliumia hapa na anakimbiliwa na docta wa timu kupewa huduma ya haraka
kazi kwako!!! ni mimi na wewe!!
Kimbiza kimbiza katikati ya uwanja, Simba wakiendesha mashambulizi
Kocha Loga..na mbwembwe mbele ya mwamuzi
No comments:
Post a Comment