Jopo
wa wang’amuzi vipaji limetangaza majina ya wachezaji 36 waliopataikana
katika mchakato wa maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha mechi za
mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema
jopo hilo liling’amua vipaji 143 katika mchakato, lakini waliochukuliwa
kwa sasa ni hao 36 tu.
Amewataja wachezaji waliochaguliwa katika
mchakato huo kwa upande wa makipa ni Abdulaziz Khatib Haji (Mjini
Magharibi), Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga), Benedicto Tinoko Mlekwa
(Mara) na Mtindi Kheri Ali (Kaskazini Unguja).
Kwa
upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao
upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter
Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba
(Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).
Mabeki wa kati ni Abbas Ali
Haji (Kaskazini Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma Namwamba (Temeke),
Hussein Juma Akilimali (Njombe), Joram Nasson (Iringa), Kayombo Silvanus
Henrico (Ilala), Miraji Maka (Mwanza), Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini
Unguja) na Said Juma Ali (Mjini Magharibi).
Viungo wapo Abubakar
Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga), Juma
Said Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga), Ryna Mgonyike (Temeke) na
Yusuf Mpilipili (Temeke).
Washambuliaji ni Abdallah Kagumbwa
(Temeke), Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Athanas Fabian
Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu (Mwanza), Ayubu Hashim Lipati (Ilala),
Chunga Said (Manyara), Mbwana Mshindo Mussa (Tanga), Michael David
Mlekwa (Lindi), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar Athuman Nyenje
(Mtwara), Paul Michael Bundala (Ilala), Ramadhan Kapalamoto (Kinondoni)
na Roman Nyapunda (Temeke).
Amesema wastani wa umri wa wachezaji hao
ambao watafanyiwa vipimo vya afya Machi 19 na 20 mwaka huu kabla ya
kambini Machi 21 mwaka huu, Tukuyu mkoani Mbeya ni miaka 21.
Timu
hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na makocha Hafidh Badru, Salum
Mayanga na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu utafanyika mchujo ili
kupata wachezaji wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa Stars
watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa Stars
inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
No comments:
Post a Comment