Pages

Tuesday, March 11, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: NI PATASHIKA LEO HII JUMANNE KWENYE MARUDIANO, BAYERN MUNICH v ARSENAL, ATLETICO MADRID v AC MILAN. JUMATANO: BARCELONA v MAN CITY, PSG v BAYER 04 LEVERKUSEN

UEFA CHAMPIONS LIGI, inarejea kilingeni kuanzia leo Jumanne Usiku kwa Mechi mbili na huko Jijini Munich, Uwanjani Allianz Arena ni Mabingwa Watetezi Bayern Munich wakiwakaribisha Arsenal na huko Spain, ndani ya Estadio Vicente Calderon, ni Atletico Madrid na AC Milan.
Kwenye Mechi hizo, Timu zote za Nyumbani, Bayern na Atletico, zipo kwenye hali njema baada ya kushinda Mechi zao za Ugenini za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kuacha kazi kubwa, hasa kwa Arsenal, kukomboa vipigo vyao.
Katika Mechi ya Kwanza huko Emirates, Arsenal ilichapwa 2-0 na Bayern Munich na huko San Siro, AC Milan ilitunguliwa 1-0 na Atletico.
UCL itaendelea Jumatano kwa Mechi nyingine mbili kati ya Barcelona na Manchester City huko Nou Camp na Paris Saint-Germain kuivaa Bayer 04 Leverkusen huko Jiijini Paris, France.
Kama ilivyo kwa Mechi za Jumanne, na Jumatano pia Timu za Nyumbani, Barca na PSG, zitaingia kwa hali njema wakiwa wameshinda Mechi zao za kwanza Ugenini kwa Barca kuipiga City 2-0 huko Etihad na PSG kuivurumisha 4-0 Bayer 04 Leverkusen huko Germany.
Mechi nyingi 4 zilizobakia za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL zitachezwa Wiki ijayo, Jumanne Machi 18 na Jumatano Machi 19.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na wachezaji wake leo hii asubuhi kwenye mazoeziKocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Arsene Wenger akihakikisha timu yake inafanya mazoezi ya kutosha.Bayern Munich mjiandae...Mertesacker na KoscielnyKocha nae ni mchezaji bwana....Wachezaji kutoka Ujerumani hawa....wakiteta hapa...Podolski na OzilOzil na Podolski
UEFA CHAMPIONS LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC (2-0)
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan (1-0)
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City (2-0)
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen (4-0)
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

No comments:

Post a Comment