Pages

Friday, March 28, 2014

SEVILLA 2 v REAL MADRID 1, CARLOS BACCA AWATULIZA REAL, AWAPOLOMOSHA NAFASI YA TATU!! BALE NA RONALDO WASHINDWA KUIBEBA TIMU.

Real Madrid ndio walianza kupata bao dakika ya 14 kuptia kwa mshambuliaji wao matata Cristiano Ronaldo, Kisha Sevilla wakasawazisha bao hilo dakika ya 19 kupitia kwa Carlos Bacca.
Kipindi cha pili Dakika ya 72 Sevilla Fc wanapata bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Real Madrid, Bao likifungwa na Carlos Bacca baada ya kupata pasi ya kutanguliziwa na Ivan Rakitic.
Kipigo hiki cha Real kinawashusha hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 70, Nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Atletico de Madrid wenye pointi 73 baada ya kuitungua usiku huu bao 1-0 timu ya Granada CF. Mapema Barcelona Waliinyuka bao 3-0 timu ya Celta Vigo, Bao za Barca zilifungwa na Neymar mbili na moja Lionel Messi.Ronaldo na Stephane M'Bia kwenye patashika iliyokuwa iwaache meno nje!

RATIBA/MATOKEO
Jumatano Machi 26

Barcelona 3 v Celta de Vigo 0
Rayo Vallecano 1 v Osasuna 0
Atletico de Madrid 1 v Granada CF 0
Sevilla FC  2 v Real Madrid 1

Alhamisi Machi 27 
22:00 Real Sociedad v Real Valladolid
22:00 Getafe CF v Villarreal CF
24:00 UD Almeria v Valencia
24:00 Levante v eal Betis

No comments:

Post a Comment