Pages

Sunday, March 9, 2014

FA CUP: FULL TIME!!!! MANCHESTER CITY 1 v WIGAN 2, CITY HOI KWA WIGAN....!!! JORDI GOMEZ NA JAMES PERCH WAACHA KILIO ETIHAD USIKU HUU!!! WIGAN KUUMANA NA ARSENAL NUSU FAINALI MWEZI UJAO!

Jordi Gomez celeb Manchester City Wigan FA CupMchezaji wa Wigan Jordi Gómez anaipatia bao katika dakika ya 27 kwa mkwaju wa penati na kufanya 1-0 dhidi ya Man City kwenye uwanja wao Etihad. Bao hilo limedumu mpaka timu zote kwenda mapumziko Wigan wakiwa mbele kwa bao hilo moja. Kipindi cha pili dakika ya 47 James Perch akawaongezea bao tena Wigan nakufanya 2-0 dhidi ya Man City baada ya kupata pasi safi kutoka kwa James McArthur na kuwafunga City wanaochezea kwenye uwanja wao Etihad. James Perch celeb Wigan Manchester City FA CupYaya Touré akipewa kadi ya njano kwenye dakika ya 48, Kipigo hicho cha bao 2-0 City wanachachamaa na kuongeza kasi kutaka kurudisha bao kwa haraka..
Dakika ya 53 City wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili, Yaya Touré anatoka na nafasi yake inachukuliwa na David Silva na Jesús Navas González nje nafasi yake inachukuliwa na Edin Dzeko ili waone kama watazirudisha bao hizo mbili katika kipindi cha dakika 30 zilizobaki! Nao Wigan wanafanya mabadiliko katika dakika ya 58 Callum McManaman anatoka nafasi yake inachukuliwa na James McClean. 
Kipindi cha pili dakika ya 68 Samir Nasri akaipachikia bao City baada ya kuachia shuti kali na kufanya 2-1 Baada ya kupata krosi kutoka kwa Micah Richards. Mpira umemalizika Wigan wakiwa washindi kwa bao 2-1 dhidi ya City na ushindi huu unawakutanisha Wigan na Arsenal kwenye Nusu fainali ya FA CUP mwezi ujao wa Nne. Msimu uliopita, mara baada ya kutwaa FA CUP, Siku 3 baadae, Wigan waliporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu England na sasa wako Championship wakiselelea Nafasi ya 7 na wapo chini ya Meneja Uwe Rosler, aliekuwa Straika wa Man City kwenye miaka ya nyuma.
Kocha wa Wigan akilalamika baada ya mchezaji wake kuangushwa ndani ya box.
Aguero(katikati) akikabwa na wachezaji wawili wa Wigan'Mchezaji wa Wigan Ivan Ramis kidogo amuumize mchezaji wa Manchester City Alvaro Negredo

Mchezaji Javi Garcia wa Man City akishikana shati na Callum McManaman wa Wigan kwenye kipindi cha dakika 45 za mwanzo..Martin Demichelis wa Manchester City alimwangusha ndani ya box Marc-Antoine Fortune wa Wigan Athletic
Jordi Gomez akimpelekesha kipa wa City na kumfunga penati kiurahisi..
Mashabiki wa Wigan wakishangilia kwenye Uwanja wa Etihad .
Kocha wa  Wigan Athletic Uwe Rosler akiwasalimia mashabiki na wadau wa soka uwanjani Etihad.
Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini na vingozi wenzake kwenye benchi la ufundi..

No comments:

Post a Comment