Mchezaji Seamus Coleman akishangilia bao lake la ushindi..
Mchezaji Seamus Coleman ameifanyia kitu mbaya Cardiff City baada ya kuifunga Bao la ushindi katika Dakika za Majeruhi na kuifanya Everton iibuke kidedea kwa Bao 2-1 Uwanjani Goodison Park.
Everon walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 59 la Gerard Deulofeu lililombabatiza Beki na Cardiff kusawazisha katika Dakika ya 68 kupitia Torres Ruiz.
Matokeo haya yameifanya Everton ikamate Nafasi ya 6 na Cardiff iwe Nafasi ya 19.
No comments:
Post a Comment