Pages

Saturday, February 1, 2014

RISSA RISASY KUZINDUA BENDI FEBRUARI 14, CASSA PLAZA MIKOCHENI, DAR ES SALAAM



Photo
KAMPUNI ya Rissa Risasy and Music Creation yenye makazi yake Dar es Salaam na London Uingereza itazindua bendi ya muziki wa dansi jijini Dar es Salaam, Februari 14, mwaka huu kwenye ukumbi wa Cassa Plaza uliopo Mikocheni, Dar es Salaam.

Akizungumza  jijini Rais wa bendi hiyo Rissa Risasy  alisema kuwa bendi hiyo inaitwa Rissa Risasy na inatumia mtindo wa “Sofiyanika”

“Mimi ni mwanamuziki wa siku nyingi hivyo nimeona ni bora nianzishe bendi yangu ili niweze kutoa burudani ya muziki wa dansi kwa wakazi wa Dar es Salaam na sehemu nyingine”, alisema Rissa

Pia alisema kiingilio kwenye uzinduzi huo ni 30,000 kwa VIP, 15,000 na 10,000 na burudani itaanza saa 3:00 hadi majogoo.

Rissa Risasy aliingia Tanzania mwaka 1987 baada ya kufuatwa DRC na mke wa Lovy Longomba kuanzisha Afriso Ngoma, baadae alihamia Sambulumaa band kisha Maquis na kuchukuliwa Virunga ya Kenya.

Mwanamuziki huyu ambaye maskani yake kwa sasa ni London na Dar es Salaam aliwahi kuvuma na Vidonge remix akiwa na bendi ya Virunga, Sambulumaa alishiriki katika wimbo Mayombo na akina Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa

No comments:

Post a Comment