Pages

Friday, February 7, 2014

NEMANJA VIDIC ATANGAZA RASMI KUONDOKA MANCHESTER UNITED


NAHODHA wa Manchester United Nemanja Vidic amethibitisha ataondoka Klabu hiyo mwishoni mwa Msimu huu.
Vidic, Raia wa Serbia mwenye Miaka 32, anamaliza Mkataba wake na Man United mwishoni mwa Msimu huu kwenye Klabu aliyoanza kuichezea Mwaka 2006.

Vidic alitoa Taarifa kwenye Tovuti ya Man United na kusema: “Sifikirii kubakia England kwani Klabu pekee niliyotaka kuchezea ni Manchester United. Sikutegemea kushinda Vikombe 15. Hata hivyo nimeamua kuondoka mwishoni mwa Msimu.”

Vidic, ambae alihamia Man United kwa Dau la Pauni Milioni 7 kutoka Spartka Moscow Mwaka 2006, alikuwa ndie Nahodha wakati Man United inatwaa Taji la Kihistoria la 20 la Ubingwa wa England Msimu uliopita ambao ndio ulikuwa wa mwisho wa Meneja Sir Alex Ferguson alieamua kustaafu.

Vidic aliongeza kusema: “Nimekuwa na Miaka 8 bora hapa. Muda wangu wote kwa Klabu hii ndio muda wangu bora katika mafanikio yangu maishani mwangu. Daima sitahasau Usiku ule huko Moscow [Wakati Man United wanaibwaga Chelsea na kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mwaka 2008] kumbukumbu daima zitabaki kwangu na Mashabiki!”

Zipo taarifa kuwa Vidic atakuwa Italy Msimu ujao huku Klabu za Juventus, Inter Milan na Fiorentina zikimuwinda.

No comments:

Post a Comment