Pages

Saturday, February 1, 2014

MANCHESTER UNITED YAFUNGWA NA STOKE CITY 2-1 LEO

LIVE:

Erik Pieters, Juan Mata Charlie Adam amewapatia bao Stoke City katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza kwa shuti kali kwenye uwanja wao wa Britannia. Bao hilo lilizama ndani ya lango la United baada ya Michael Carrick kumwamisha mchezaji wa United langoni.

Mpaka mapumziko timu Stoke walikuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya United huku mchezaji wao Phil Jones akiumia na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Danny Welbeck.

Kipindi cha pili dakika ya 47 United wanasawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Robin Van Persie.
Dakika ya 51 Adam akachia shuti kali lililompita mlinda mlango wa United De Gea na kutinga moja kwa moja hadi langoni na kufanya Stoke watangulie kwa bao 2-1.

No comments:

Post a Comment