Pages

Tuesday, February 4, 2014

JOSE MOURINHO ALIPOMTOA KIJASHO KOCHA WA CITY MANUEL PELLEGRINI AKITUMIA MBINU ZA KUSHAMBULIA NA KUTUPIA MBALI

Chelsea Jose Mourinho amemshangaza kila Mtu kwa mbinu alizotumia katika kuibwaga Manchester City Bao 1-0 Uwanjani Etihad katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Jumatatu Usiku.
Kimtazamo Timu aliyopanga Mourinho ilionekana ni ya kujihami lakini Uwanjani Kikosi chake kilishambulia kinyume na matarajio ya wengi na kumhadaa kabisa Meneja wa Man City Manuel Pellegrini.
Alipohojiwa kabla ya Mechi kama Kikosi alichopanga ni cha ‘Kupaki Basi’, Mourinho alijibu: “Kupaki Basi hakuhusiani na Kikosi Meneja anachochagua bali ni jinsi unavyocheza. Unaweza kucheza na Wachezaji 6, 7, 8 wa Difensi lakini ukawa na Timu inayoshambulia!”
Na hiyo ndio ilikuwa Plani ya Mourinho. 

Kwa kutomchezesha Kiungo Mchezeshaji, Oscar, na kuwatumia Viungo David Luiz, Nemanja Matic na Ramires, Mourinho alikuwa akitumia Mfumo wake wa Kujihami wa 4-3-3 aliopata nao Sare ya 0-0 huko Emirates alipokumbana na Arsenal kabla ya Krismasi.

Lakini safari hii, Chelsea walikwenda mbele, walishambulia na walisaidiwa sana kwa City kumkosa Majeruhi Fernandinho na kumtumia Martín Demichelis kitu ambacho kilimfanya Mourinho amweke Willian Kiungo wa kati.
Mtu 3 za David Luiz, Matic na Ramires ziliweka ngao nzuri kwa Difensi ya Chelsea na kumtuliza David Silva ambae, bila ya kuwepo Sergio Agüero, Samir Nasri na Fernandinho, alihitajika kuwa mbunifu zaidi lakini alishindwa kuwa hivyo.


Timu zote mbili zilitumia Winga moja kushambulia zaidi huku City wakimtegemea Fulbeki Aleksandar Kolarov kupanda juu na aliweza kupiga krosi kadhaa kwa Yaya Touré na Silva kufunga na wakashindwa. 
Upande huo huo, Chelsea walikuwa na Fulbeki Branislav Ivanovic ambae, tofauti na Mechi nyingine, safari hii alipanda juu sana na kuelekeza Mashambulizi na kila akipanda juu Viungo, David Luiz na Matic, walikuwa wakiziba pengo lake.


Moja ya Mashambulizi ya Ivanovic ndio yalizaa Goli baada kupanda na kufumua Shuti kali nje ya Boksi kwa Guu la kushoto na kuifungia Chelsea Bao la ushindi.

Hakika huo ulikuwa Mchezo safi sana kwa Chelsea wakati Wachezaji wa kujihami walishambulia na wale Washambuliaji walianza ulinzi huko huko mbele.
Stamina ya Willian, aliekuwa akizunguka kote katikati kuwabana Viungo wa City, ilikuwa ni kitu muhimu kwenye ushindi wao ambao ulichangiwa pia na Hazard kujituma mno na hata kurudi nyuma kukaba.


Huu ulikuwa ushindi mkubwa mno kwa Mourinho kwa jinsi alivyotumia mbinu na mikakati bora kuwashangaza wengi, na hasa Manuel Pellegrini.

No comments:

Post a Comment