Pages

Sunday, February 9, 2014

BARCELONA YAIFUNGA SEVILLA 4-1 KWENYE LA LIGA NA KURUDI KILELENI


Leo Barcelona wakicheza ugenini Sevilla wameifunga bao 3-1 timu ya Sevilla. Sevilla ndio walianza kupata bao dakika ya 15 kwa shuti kali la Alberto, Baadae dakika ya 34 Alexis akasawazisha baada ya kupigwa fri kiki na Lionel Messi na hatimae Alexis kujitwisha mpira wa kichwa mpaka langoni mwa lango la Sevilla huku Sevilla wakibaki kuduwaa. Dakika ya mwisho mwa kipindi cha kwanza katika dakika ya 44 Barcelona wakapata bao baada ya kufanya shambulizi la kushtukizia na bao hilo likifungwa na Staa Lionel Messi kwa shuti kali. Na mpira kumalizika kwa kipindi cha kwanza Barcelona wakiwa juu ya bao 2-1 dhidi ya wenyeji Sevilla.
Kipindi cha pili uwanja ukiwa na maji baada ya mvua kunyesha kwa muda katika dakika ya 56 Lionel Messi akafunga bao la tatu na kufanya mabao kuwa 3-1.

Dakika za lala salama dakika ya 88 Cesc Fábregas aliyetokea benchi kwa kuchukua nafasi ya Pedro katika dakika ya 73 akawaongezea bao Barcelona na kufanya 4-1 

Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Sevilla

Messi tena akiifanyia Barcelona 3-1 dhidi ya wenyeji Sevilla
Mapema kipa Victor Valdes alifungwa na  Alberto Moreno katika dakika ya 15

Wachezaji wa  Sevilla wakipongezana baada ya kupata bao wakiwa wa kwanza.

 Piotr Trochowski na Sanchez kwenye patashika

Hakunaga!!! Tupo kileleni tena leo!!!

Meneja wa Barcelona  'Tata' Martino akitoa maelekezo leo

Messi  leo kafikisha mabao 334, na hapa akishukuru kwa yote!!

No comments:

Post a Comment