Pages

Monday, February 3, 2014

ARSENAL 2 CRYSTAL PALACE 0, BAO ZA ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN ZAIRUDISHA GUNNERS KILELENI

Kipindi cha kwanza kimemalizika timu zote zikiwa 0-0, hakuna aliyeliona lango la mwenzake. Arsenal wakipata kona 3 na Crystal Palace wakipata kona 1 tu. 
Kipindi cha pili dakika ya 47 mchezaji Alex Oxlade-Chamberlain akaipatia bao Arsenal baada ya yeye kubaki na kipa kumfunga kwa kupaisha mpira juu na kufanya 1-0. Dakika ya 72 mchezaji huyo huyo Alex Oxlade-Chamberlain amekatiza katikati ya mabeki wa Crystal Palace na kuachia shuti kali na kumfunga kipa wao bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Crystal Palace kwenye uwanja wa Emirates.
Bao hizo mbili za Alex zilidumu mpaka dakika 90 za mchezo na kufanya Arsenal waibuke na ushindi wa bao 2-0, Ushindi huu wa Arsenal umewarudisha tena kileleni wakiwa na pointi 55 juu ya Chelsea na Manchester City. Man City Kesho jumatatu wanaikaribisha Chelsea kwao Etihad na kama City watashinda watakaa kileleni. Pia Chelsea wakiweza kuwazima City watakuwa katika nafasi ya pili wakilingana na City.Marouane Chamakh akicheza na timu yake ya zamani ArsenalKocha mkuu wa Crystal Palace Tony Pulis akiwapa maelekezo uwanjani vijana wakeOlivier Giroud akikabwa na mchezaji wa Crystal Palace Mile JedinakMajanga kipa na Sagna
Nakatiza hapa!!..Mashabiki wa Gunners wakipitiwa na jua

No comments:

Post a Comment