Pages

Monday, February 3, 2014

ANDERSON AITUPIA NENO MANCHESTER UNITED!

Anderson, ambae Wiki iliyopita alijiunga na Fiorentina ya Italy kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu kutoka Manchester United, amesema hana nia ya kurudi Old Trafford na pia kudai Mastaa wengi wataihama Man United.
Kwa mujibu wa Anderson, Mastaa ambao wataondoka Man United ni pamoja na Winga wa Ureno, Nani, ambae mwanzoni mwa Msimu huu alisaini Mkataba mpya wa Miaka mitano na Man United.
Anderson amesema: “Nina hakika Wachezaji wengi wanataka kuondoka, hasa mie na Nani ambao tulikuwa huko Miaka 7 au 8. Manchester United ni Klabu kubwa, Klabu inayotimiza kila kitu kwa Wachezaji wake, lakini mara nyingine Mchezaji anataka kuhama ili kupata uzoefu mwingine na kujifunza mengine.”

Hata hivyo, ndani ya Man United, inajulikana kuwa Rio Ferdinand, Patrice Evra na Nemanja Vidic wanamaliza Mikataba yao mwishoni mwa Msimu huu huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hatima ya Nani na Javier Hernandez ‘Chicharito.’

No comments:

Post a Comment