Pages

Saturday, February 1, 2014

ALEX MICHAEL AWA BONDIA BORA WA DABA




BONDIA Alex Michael wa klabu ya JKT Mgulani anayepigana kwenye uzani wa kg 60 amekuwa bondia bora wa mashindano ya ngumi mkoa wa Dar es Salaam yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Panandi, Ilala Bungoni.

Mashindano hayo ambayo yalianza Januari, 27 yalimalizika juzi kwa jumla ya mapambano 48 kuchezwa ikiwepo ya wanawake na watoto.
Akizungumza baada ya mashindano hayo kumalizika, Mwenyekiti wa Chama cha ngumi za Ridhaa, mkoa wa Dar es Salaam, (DABA) Karoly Godfrey, alisema kuwa mashindano hayo yalimefana na yamesaidia kujua na kujionea vipaji vingi katika mkoa wa Dar es Salaam.

“Lengo la mashindano limefanikiwa kwani mabondia wengi wameshikiriki kwa sababu mkoa wa Dar es Salaam una takribani miaka mitatu bila kuandaa mashindano ya ngumi na haya ni mashindano ya kwanza kwa uongozi wetu kuandaa tangu tuingie madarakani mwaka jana”, alisema Godfrey

Pia alisema wana changamoto za vifaa hali inayofanya kuchelewesha muda wa mchezo kusubiri mabondia kubadilishana hivyo wanaomba wadau kuwasaidia ili kuinua mchezo huo.

Katika mchezo wa fainali uzito wa kg 49, bondia Mussa Mchomamnga alishinda  baada ya mwamuzi kumwokoa bondia Antony Idoa kutokana na kuzidiwa  na bondia Hafidh Bamtula alishinda kwa pointi mbili kwa moja dhidi ya bondia George Constatino hali iliyozua malalamiko kwa mmoja wa jaji wa mchezo huo alikuwepo baba mzazi wa Hafidh Bamtula.

Kwenye uzito wa kg 56 bondia Emilian Patrick alishinda kwa pointi mbili kwa moja dhidi ya bondia Frank Nicholaus, mchezo ambao uliwazutia wengi kutokana na ufundi wa kurushiana ngumi kwa zamu.

Bondia Alex Michael alishinda kwa pointi Yousole Said kwenye pambano la uzito wa kg 60 na Victor Njaiti alishinda kwa pointi dhidi ya Haruna Husein kwenye pambano la uzito wa kg 64.

Naye bondia Mohamed Chibumbui alimpiga Abdul Ashid kwa pointi mbili kwa moja kwenye pambano la kg 69, huku Hamad Halfan akimpiga kwa KO bondia Salum Jafari kwenye pambano la kg 75.

Naye mwanadada Ellen Mushi alimpiga Siwatu Kimbe kwa pointi mbili kwa moja kwenye pambano la raundi nne huku Sarah Andrew akimpiga Grace Michael kwa pointi kwenye pambano la raundi nne pia.

No comments:

Post a Comment