Pages

Friday, January 3, 2014

TEMEKE KUCHEZA FAINALI NA MOROGORO KESHO MASHINDANO YA NETBOLI TAIFA CUP






Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan akiwasalimu wachezaji wa timu ya Kinondoni

Mbunge wa Kinondoni akiwasalimu wachezaji wa Temeke

Mbunge wa Temeke Abass Mtemvu akiteta jambo na wachezaji wa Temeke wakati wa mapumziko

Idd Azan naye hapa anajitahidi kuteta na wachezaji wa Kinondoni wakati wa mapumziko baada ya kuona jahazi zinazama

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akimkabidhi Katibu wa Chaneta, Anna Kibira, pesa taslimu 1,000,000

Baadhi ya wadau waliokuwepo
TIMU za mchezo wa pete ya mkoa wa Temeke na Morogoro  zimeingia fainali ya mashindano ya Taifa Cup, baada ya kushinda michezo yao leo iliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Temeke ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo walianza kuliandama lango la Kinondoni tangu robo ya kwanza ya mchezo kwani walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 14 na Kinondoni wakiwa na mabao 9.

Kama vile haitoshi huku kila timu ikihamasisha na mbunge wake, Temeke wakiwa na Abbas Mtemvu huku Kinondoni wakiwa na Idd Azan waliendelea kuoneshana ushindani lakini Temeke waling’aa zaidi baada ya kuifunga Kinondoni  mabao 16 kwa 9.

Kwenye robo ya tatu Kinondoni walipotea kabisa na kujikuta wakifungwa mabao 17 kwa 5 na robo ya nne ya kukamilisha mchezo Kinondoni walizidi kuelemewa baada ya kupokea kipigo cha mabao 19 kwa 10.
Kinondoni hawatamsahau GS wa Temeke Mwanaidi Hassan kwani ndiye alikuwa mwiba mchengu kwa kutumbukiza mabao mengi  katika mchezo wao.

Nusu fainali ya pili ilizikutanisha timu za Morogoro na Katavi ambapo Morogoro ndiye atakayecheza fainali na Temeke baada ya kuifunga Katavi mabao 50 kwa 29.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alisema kuwa Temeke wanafanya vizuri na watatetea ubingwa wake kutokana na maandalizi mazuri walioyafanya huku mbunge wa Kinondoni, Idd Azan akizitaka halmashauri kusaidia timu zinazowakilisha mikoa kwani zina mafungu maalum kwa ajili ya michezo.

Naye Katibu wa Chama cha Netbali (CHANETA) Anna Kibira alimpongeza na kumshukuru Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kwa jinsi alivyojitoa kukisaidia Chama cha Netbali  na kuomba wadau wengine kujitokeza kuinua mchezo huo ambao unatoa ajira kwa vijana.

‘Namshukuru Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kwani leo ametimiza ahadi yake ya kukisaidia CHANETA 1,000,000 ambazo amekabidhi mbele yenu hivyo naomba watu wengune na makapuni yasaidie mchezo huu kwani unatoa ajira kwa vijana”, alisema Kibira.

No comments:

Post a Comment