Nemanja Matic amehamia Chelsea kwa Dau la Pauni Milioni 21.
Matic, Miaka 25 na Raia wa Serbia, ni Kiungo wa Benfica ya Ureno na anategemewa kurudi tena Stamford Bridge baada kuondoka Miaka mitatu iliyopita alipotolewa kafara ili Chelsea imsaini Beki wa Brazil David Luiz kutoka Benfica.
Matic alijiunga na Chelsea akitokea Klabu ya Slovakia, MFK Kosice, Mwaka 2009 kwa Dau la Pauni Milioni 1.5 na kuichezea Chelsea Mechi mbili tu akitokea Benchi.
Matic amemwaga wino kwa kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu na Klabu ya Chelsea
No comments:
Post a Comment