Pages

Tuesday, January 28, 2014

MASHINDANO YA NGUMI MKOA WA DAR ES SALAAM YAANZA



Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindan ya  wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa pointi
Mwenyekiti wa Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es salaam DABA akimkabidhi risara Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu wakati wa mashindano ya wazi yaliyoanza jumatatu
Mbunge wa Ilala (kushoto|) akifuatilia masumbwi

Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala (kuliaakimtupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoendelea katika ukumbi wa panandi Panandi Ilala Bungoni, Ibrahimu alishinda kwa pointi
SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa Mkoa wa Dar es salaam umezindua rasmi mashindano yake ya kwanza tangia waingie Madarakani mashindano hayo yalifunguliwa jana.
Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu ambayo imekutanisha zaidi ya timu ishirini na mabondia 60 wa mkoa huu akisoma risala kwa mgeni rasmi 

Mwenyekidi wa ngumi mkoa wa Dar Akaroli Godfrey amesema mbali na mashindano hayo kuwa na changanmoto mbalimbali wameamua kuyafanya kwa kuwa yapo kwenye kalenda yao ata hivyo hakuna zawadi zozote kwa mabondia watakaopigana hivyo kama mbunge wa jimbo la Ilala tunaomba utupatie angalau medali kwa mabondia aidha vifaa tulivyo navyo havikidhi kimchezo

akijibu lisara hiyo mbunge huyo ame haidi kutoa zawadi pamoja na kuwa mlezi wa ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es salaam na kuwasaidia kutafuta wadhamini mbalimbali watakaojitokeza kuinua mchezo wa masumbwi nchini ili ngumi zisonge mbele 

Katika ufunguzi huo mabondia Anton Idoa alimtwanga kwa KO ya raundi ya pili bondia Mohamed Mzeru huku John Cristian akimsambaratisha Omar Said, na shabani Alimasi akimdunda Saidi Kondo na bondia pekee kutoka timu ya shanti ya Ilala,Hussein Pendeza alipoteza kwa pointi na Ayubu Ibrahimu  
 
 

No comments:

Post a Comment