Pages

Wednesday, January 1, 2014

MANCHESTER UNITED KUCHEZA NA TOTTENHAM HOTSPURS BILA STAA ROONEY WALA VAN PERSIE

MABINGWA MANCHESTER UNITED huenda wakacheza Mechi ya Mwaka mpya dhidi ya Tottenham bila ya Mastraika wao wakubwa kwa mara nyingine tena kama alivyotoboa Meneja wao David Mpyes.
Robin van Persie amekuwa nje ya Uwanja kwa Mechi 5 sasa akijiuguza Paja lake na Wayne Rooney aliikosa Mechi ya Jumamosi walipoifunga Norwich City Bao 1-0 akiwa na tatizo la Nyonga.
Ingawa Robin van Persie ameshaanza tena Mazoezi lakini Mechi hii na Tottenham Jumatano Usiku Uwanjani Old Trafford huenda ni mapema mno kwake wakati Rooney atasubiri apimwe Dakika za mwisho kabla ya Mechi ili kuthibitisha kama yuko fiti kabisa.
Akiongea na Wanahabari katika Mahojiano maalum kabla ya pambano na Tottenham, David Moyes alisema: “Inabidi tusubiri na kuona kuhusu Wayne. Hakufanya Mazoezi Jumatatu hivyo inabidi tutathmini na tujue hali iko vipi. Robin bado hajawa tayari lakini tunategemea hayuko mbali sana.”

Kukosekana kwa Mastraika hao wawili kutafanya Danny Welbeck, ambae ndie alifunga Bao la ushindi huko Carrow Road dhidi ya Norwich, na Javier Hernandez ‘Chicharito’ wawe na jukumu la kuipa Man United ushindi wao wa 7 mfululizo lakini David Moyes amepoza matumaini makubwa ya kuibuka upya.Amesema: “Sidhani kama kuna Mtu anajirusharusha kwa furaha kwa sababu tumeshinda Mechi 6 mfululizo-hapa ni kitu kinachotegemewa!”

Aliongeza: “Tottenham ni wapinzani wagumu! Siku zote ni Timu nzuri na ngumu!”
Kwa sasa Tottenham inaongozwa na Tim Sherwood baada ya kutimuliwa Andre Villas-Boas hapo Desemba 16 na tangu wakati huo, Sherwood amemudu kuiongoza Tottenham kuifunga Southampton 3-2, Sare na West Brom na ushindi dhidi ya Stoke City.
Hivi sasa Tottenham wako nyuma tu ya Man United kwenye Msimamo wakiwa na Pointi sawa lakini wamezidiwa kwa ubora wa Magoli.


RATIBA MECHI ZA LEO
Jumatano Januari 1

15:45 Swansea vs Man City
18:00 Arsenal vs Cardiff
18:00 Crystal Palace vs Norwich
18:00 Fulham vs West Ham
18:00 Liverpool vs Hull
18:00 Southampton vs Chelsea
18:00 Stoke vs Everton
18:00 Sunderland vs Aston Villa
18:00 West Brom vs Newcastle
20:30 Man United vs Tottenham

No comments:

Post a Comment