Pages

Saturday, January 18, 2014

GHANA KUCHEZA NA LIBYA KUNDI C

  Leo timu za taifa za Ghana na Libya zitakuwa zikishuka dimbani kusaka nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ya fainali za mataifa ya Afrika ya CAF watakapokuwa wakishuka katika dimba la Free State Stadium.
Mataifa yote hayo mawili yalishinda katika michezo yao ya ufunguzi Jumatatu usiku mjini Bloemfontein.
Ushindi kwa yoyote baina yao itakuwa unawapa nafasi ya kusonga mbele katika robo fainali ya michuano hiyo na la muhimu zaidi kumaliza katika nafasi ya juu katika kundi C.
Mshindi wa kwanza wa kundi hili atakutana dhidi ya mshindi wa nafasi ya pili wa kundi D, kundi ambalo linaonekana kama mchekea katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment