Pages

Wednesday, January 1, 2014

FRANCIS MIYEYUSHO AMTWANGA JOSHUA AMAKULU KWA KO MSASANI CLUB
















BONDIA Francis Miyeyusho jana aliwapa raha ya kufunga mwaka watanzania baada ya kumpiga kwa KO bondia Joshua Amakulu wa Kenya katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika katika Ukumbi wa Msasani beach, Kinondoni.

Katika pambano hilo Miyeyusho alimpiga Amakulu kwa KO raundi ya pili na kufanya ukumbi ulipuke kwa nderemo na vifigo huku kila mtu akimpongeza Miyeyusho kwa kazi nzuri ya kumpiga mpizani kabla ya kumaliza raundi zote 10.

Awali Miyeyusho alikuwa apigane na David Charanga toka Kenya lakini bondia huyo alifiwa na mama yake mzazi akalazimika kutofika ndipo akaja Amakulu aliyepokea kipigo cha mbwa mwizi.

Katika mapambano ya utangulizi  bondia Ibrahimu Class 'King Class alimpiga Mustafa Dotto kwa pointi katika pambano ambalo lilikuwa laraundi sita 
Bondia Kalama Nyilawila alimpiga kwa KO kwenye raundi ya pili kwenye pambano la raundi

Bondia Iddy Mnyeke  na Cosmas Cheka walitoka sare katika pambano lililokuwa la raundi sita. 

Akizungumza baada ya mpambano huo Francis Miyeyusho alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa kushinda pambano hilo pia kwa sapoti kubwa aliyoipata toka kwa viongozi na mashabiki wa ngumi.

No comments:

Post a Comment