Pages

Tuesday, January 28, 2014

CHAN 2014: RATIBA YA NUSU FAINALI, JUMATANO NI ZIMBABWE vs LIBYA, GHANA vs NIGERIA

NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29

18:00 Zimbabwe v Libya [Free State Stadium]
21:30 Ghana v Nigeria [Free State Stadium]

Jumamosi Februari 1
18:00 Mshindi wa Tatu [Cape Town Stadium]
21:00 Fainali [Cape Town Stadium] 

Wachezaji wa Nigeria

Robo Fainali za CHAN 2014, Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Nchi zao tu, zimekamilika kwa Libya na Ghana kufuzu kuingia Nusu Fainali na kuungana na Zimbabwe na Nigeria waliofuzu Jumamosi.
Kwenye Mechi ya Awali, Dakika 90 za Robo Fainali kati ya Gabon na Libya ilimalizika kwa suluhu ya 1-1 baada Libya kutangulia kufunga katika Dakika ya 50 kupitia Abdelsalam Omar na Daniel Cousin kuisawazishia Gabon Dakika ya 74 kwa Penati baada ya Fetori kumvuta Lionel Yackouya na Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 bila mabadiliko.
Kwenye Mikwaju ya Penati, baada Dakika 120, Libya walitoka Washindi kwa Penati 4-2 baada kufunga Penati zao zote 4 na Gabon kukosa 2 na kutinga Nusu Fainali ambapo Jumatano watacheza na Zimbabwe.
Katika Mechi iliyofuatia, Penati ya Dakika ya 68 ya Kwabina Adusei imewapeleka Ghana Nusu Fainali baada ya kuifunga Congo DR Bao 1-0.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Kimwika wa Congo DR kuunawa Mpira kwenye Boksi.
Kwenye Nusu Fainali Jumatano ijayo, Ghana watawavaa Wapinzani wao wa Jadi Nigeria.

Kudakwashe Mahachi wa Zimbabwe akishangilia baada ya timu yao kwenda katika hatua ya nusu Fainali huko Africa Kusini.

No comments:

Post a Comment