Pages
▼
Tuesday, December 31, 2013
YANGA YAOGOPA MAPINDUZI CUP, TIMU KUTOSHIRIKI
Uongozi wa klabu ya Young Africans umewasilisha barua rasmi kwa ZFA kutoshiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Januari Mosi 2014 Visiwani Zanzibar katika miji ya Unguja na Pemba kutokana na kuamua kulivunja benchi nzima la Ufundi.
Kufuatia kupewa taarifa (notice) kwa kocha msaidzi Fred Felix "Minziro" kocha wa makipa Razaki Siwa na daktari wa timu Nassoro Matuzya kwa sasa Young Africans haina kiongozi wa benchi la ufundi hali inayopelekea timu kujitoa katika mashindano hayo.
Wiki iliyopita mholanzia Ernie Brandts alipewa taarifa (notice) ya siku thelathini (30) na klabu ya Young Africans kusitisha mkataba wake na timu ilikuwa chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa ambao nao pia wamepewa taarifa za kusitisha ajira zao.
Kutokana na timu kwa kwa sasa kutokua na kocha mkuu, kocha msaidizi, kocha wa makipa na dakatari wa timu imekua ni vigumu kwa kikosi cha Young Africans kwenda kushiriki mashindano hayo kwani haina mwalimu hata mmoja kwa sasa.
Hii inafuatia uongozi wa klabu ya Young Africans kuamua kufanya mabadiliko ya benchi zima la Ufundi kwa lengo la kuongeza tijaa katika utendaji na kuhakikisha benchi linapata watu wa kuchukua nafasi zao na kuanza kazi mara moja.
Aidha uongozi unaendelea na mchakato wa kuwapata warithi watakaochukua nafasi hizo haraka ili waweze kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Idadi ya makocha waliotuma maombi ya kuomba kuinoa timu ya Yanga mpaka sasa ni 45 huku pia idadi hiyo ikiendelea kuongeza kadri siku zinavyokwenda na uongozi unaamini utapata makocha wazuri, wenye uwezo mkubwa pia wa kuifikisha Yanga katika hatua nyinge ya juu zaidi.
No comments:
Post a Comment