Pages

Saturday, December 7, 2013

RATIBA - COPA DEL REY:RAUNDI YA 4, BARCELONA vs CARTAGENA, OLYMPIC XATIVA vs REAL MADRID, SANT ANDREU vs ATLETICO MADRID.

TIMU vigogo, Barcelona, Real Madrid na Mabingwa Watetezi Atletico Madrid, wote wanaanza kampeni zao kwenye Kombe la Mfalme huko Spain, Copa del Rey, kwa kucheza Ugenini na Timu za Madaraja ya chini. 

Mechi hizi ni za Raundi ya 4, Raundi ya Timu 32, ambazo Timu hucheza Nyumbani na Ugenini, na Vinara wa La Liga, Barcelona, wanacheza Ijumaa Usiku Ugenini na Klabu ya Daraja la Segunda B, Cartagena. 
Barca wanaingia kwenye Mechi hii wakitoka kwenye vipigo viwili mfululizo walivyopigwa na Ajax kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na kufuatia kile cha Athletic Bilbao kwenye La Liga.
Hali hii itamfanya Kocha Gerardo Martino kuchezesha Kikosi imara ili kuepuka kufungwa kwa mara ya tatu mfululizo wakati alianza vyema Barca akiwa hajafungwa hata Mechi Msimu huu.

Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Atletico Madrid, ambao huenda wakakutana na Watani zao Real Madrid kwenye Nusu Fainali ya Kombe hili ikiwa wote watafuzu, Jumamosi wapo Ugenini kucheza na Sant Andreu, Timu ya Daraja la Tatu.
Atletico Madrid, chini ya Kocha Diego Simeone, walitwaa Copa del Rey Mwezi Mei kwa kutinga Fainali bila kufungwa na kuichapa Real Madrid 2-1 na kutwaa Kombe ikiwa mara yao ya 10.
Nao, Real Madrid, wapo Ugenini kucheza na Olimpic Xativa ambayo ipo Daraja la Segunda B wakiwa Pointi 5 tu juu ya Kikosi C, Timu ya 3, ya Real Madrid.
Lakini afueni kwa Olimpic Xativa ni kuwa Cristiano Ronaldo hatacheza Mechi hii kwa vile yupo Kifungoni baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwenye Fainali ya Kombe hili Real walipofungwa na Atletico Mwezi Mei.

RATIBA
Ijumaa Desemba 6
14:00- Lleida v Real Betis
18:00 Villarreal v Elche
20:00 Algeciras v Real Sociedad
22:00 Racing Santander v Sevilla
24:00 Valladolid v Rayo Vallecano
24:00 Cartagena v Barcelona
Jumamosi Desemba 7
18:00 Sant Andreu v Atletico Madrid
20:00 Girona v Getafe
22:00 Celta Vigo v Athletic Bilbao
24:00 Olimpic Xativa v Real Madrid
24:00 Recreativo Huelva v Levante
Jumapili Desemba 8
14:00 Alcorcon v Granada
19:00 Gimnastic v Valencia
19:00 Las Palmas v Almeria
21:00 Real Jaen v Espanyol
23:00 Malaga v Osasuna

No comments:

Post a Comment