Pages

Monday, December 30, 2013

PAN AFRICAN WATAKIWA KUFUATA NGAZI HUSIKA NA MKUTANO WA WAANDISHI JB BELMONTE

Wanachama wa Pan African wametakiwa kufuata ngazi husika pale wanapoona viongozi wa klabu yao wanakwenda kinyume na Katiba yao.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imetoa mwongozo huo kwa wanachama wa Pan African baada ya kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulalamikia uongozi wao wakati wao si wanachama wa TFF.

Wanachama hao wanalalamikia uongozi wa klabu yao kwa kuitisha mkutano wa uchaguzi kabla ya ule wa kawaida ambao unatakiwa kufanyika mara moja kwa mwaka.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imelazimika kutoa mwongozo huo kwa vile wanachama hao katika malalamiko yao wamekigusa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambacho ni mwanachama wa TFF.

Pan African ni mwanachama wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDFA) ambao ndiyo wanachama wa DRFA. Hivyo, TFF imemtaka mwanachama wake DRFA kupitia IDFA kufuatilia tatizo hilo na kulipatia ufumbuzi.

MKUTANO WA WAANDISHI JB BELMONTE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitisha Mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika Desemba 31, 2013 saa 6 kamili mchana.

Mkutano huo utafanyika kwenye hoteli ya JB Belmonte iliyoko Jengo la NSSF Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment