Pages

Thursday, December 26, 2013

MANCHESTER UNITED YAWAPA MASHABIKI WAO ZAWADI YA BOXING DAY KWA KUIFUNGA HULL CITY 3-2

Mchezaji alieanzia Soka lake huko Old Trafford James Chester, ameifanya Manchester United itokenyuma kwa Bao 2-0 na kushinda Bao 3-2 Uwanjani KC baada ya kujifunga mwenyewe Bao la 3 katika Dakika ya 66.
Chester ndie alieipa Hull Bao la kuongoza na ndani ya Dakika 13 waliongoza Bao 2-0 baada ya Shuti hafifu la David Meyler kumbabatiza Jonny Evans na kumhadaa Kipa De Gea.
Lakini Man United walizinduka na Chris Smalling kuunganisha kwa kichwa frikiki nzuri ya Wayne Rooney na kufunga Goli la Kwanza na Dakika 7 baadae Wayne Rooney aliisawazishia Man United kwa Bao tamu baada kusogezewa na Danny Welbeck.


Hilo ni Bao la 150 kwa Rooney kwenye Mechi za Ligi akiwa na Man United na kumfanya awe Mechezaji wa Pili kufikisha idadi hiyo akichezea Klabu moja tu na mwingine ni Thiierry Henry aliekuwa Arsenal na kufunga Bao 175.
Hadi Haftaimu Bao zilikuwa 2-2 na ndipo Kipindi cha Pili Chester alipojifunga kwa kichwa baada kuicheza krosi ya Ashley Young iliyokuwa ikielekea kwa Rooney.
Valencia alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Dakika ya 90 baada kupewa Kadi ya Njano ya Pili kwa kupoteza muda kwa makusudi.

Valenciaakioneshwa kadi nyekundu na kutolewa nje......nje!!!...kutoka 2-0 mpaka 2-3!!! hivi kwa nini??? kocha wa Hull akijiuliza hapa kipindi cha kwanza!Jamani jitahidini nafa mieee...Juu ya kuti kavu.....Kibarua changu si... nilikuwa nimeishakuwa mbele kwa bao 2-0 lakini!!!Siamini hata kidogo!!Young akijaribu kumfunga kipa wa Hull City Rooney akifunga bao kwa shuti la mbaliRooney kwenye patashika kuusaka mpira akikwaana na mchezaji wa HullSmalling akishangilia bao lake Dakika ya 19 Smalling akitupia kwa kichwa!! Hull ndio walianza kutangulia mapema dakika ya 4 likiwa bao la  kizembe kwa Unitedsafi...tupongezane!!!De  Gea akipitwa na mpira langoni..Chester akitupiajamani jamani....mpira ukiziona nyavu kwa De GeaDe Gea kama siku zote hapendi kufungwa hapa alikuwa akishangaa shangaaMwenyekiti Assem Allam akisalimiwa Sir Alex Ferguson nae alisafiri kwenda kuutazama mpira wa timu yake ya zamani uliochezwa kwenye uwanja wa KC. United wakishinda bao 3-2 dhidi ya wenyeji Hull City.

RATIBA/MATOKEO:
Alhamisi Desemba 26

Hull City 2 Man United 3 FT
Aston Villa 0 v Crystal Palace 1
Cardiff 0 v Southampton 3
Chelsea 1 v Swansea 0
Everton 0 v Sunderland 1
Newcastle 5 v Stoke 1
Norwich 1 v Fulham 2
Tottenham 1 v West Brom 1
West Ham 1 v Arsenal 3


20:30 Man City v Liverpool

No comments:

Post a Comment