Pages

Sunday, December 22, 2013

KOMBE LA DUNIA: BAYERN MUNICH YAIBUKA BINGWA, AICHAPA RAJA CASABLANCA BAO 2-0

Bayern Munich wamekamilisha Mwaka mwema wa 2013 kwa kutwaa Taji la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu kwa kuifunga Bao 2-0 Raja Casablanca ya Morocco katika Fainali iliyochezwa Jana Usiku huko Stade de Marrakech, Marrakesh, Nchini Morocco.
Bao za Bayern zilifungwa na Dante baada ya Dakika 7 na Thiago Alcantara katika Dakika ya 22.
Hili ni Taji la Tatu kwa Klabu Duniani kwa Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola, ambaeametwaa mawili akiwa na FC Barcelona.

Hadi sasa Bayern Munich wanashikilia Mataji ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Bundesliga, German Cup na Uefa Super Cup.

Katika Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu iliyochezwa awali kabla Fainali, Atletico Mineiro ya Brazil iliifunga Bao 3-2 Guangzhou Evergrande ya China na Staa wa Brazil Ronaldinho alipewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 87.

Dante celebrates na wenzie wakishangilia baada ya kufunga goli

Mpaka ndani ya nyavu kiurahisi....

2-0: Thiago akifunga bao David Alaba akishangilia

Meneja Manager Pep Guardiola kwenye mshangao baada ya timu kufanya vema huko Morocco

Dante kidogo agunge bao jingine hapa baada ya kupigwa kona...

Mashabiki wa Bayern huko Morocco wakishangilia kwa aina yao baada ya kuona wako mbele na dakika zikizidi kuyoyoma

No comments:

Post a Comment