Pages

Sunday, December 29, 2013

KEVIN-PRINCE BOATENG ASHAMBULIWA UJERUMANI

Polisi wanachunguza tukio ambapo kiungo wa timu ya taifa ya soka ya Ghana Kevin - Prince BOATENG alishambuliwa mnamo Siku Kuu ya Krismasi baada ya kuzuka ugomvi katika eneo la Kaarst nchini Ujerumani 
Polisi karibu na mji wa Düsseldorf wamethibitisha tukio hilo wakisema Boateng mwenye umri wa miaka 26 alishambuliwa akiwa barabarani na mtu ambaye hakutambulika. Kiungo huyo anayechezea klabu ya Schalke 04 alipata majeraha madogo tu.
Gazeti la michezo la Bild liliripoti kuwa Boateng alimtembelea mtoto wake wa kiume, nyumbani kwa mkewe wa zamani, mnamo Siku ya Krismasi, wakati alipopigwa na mtu mmoja ambaye hakutambulika na akaanguka.
Boateng alizaliwa mjini Berlim na akaichezea Ujerumani katika kila kiwango, lakini anaichezea timu ya taifa ya Ghana ambao wamepangwa na Ujerumani, Ureno na Marekani katika Kundi G la dimba la Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka wa 2014.

No comments:

Post a Comment