Pages

Tuesday, December 3, 2013

CHELSEA ILIVYOIFUNGA SOUTHAMPTON 3-1,WASOIGELEA KARIBU ARSENAL KILELENI

Chelsea na Manchester City leo zimeshinda Mechi zao za Ligi Kuu England walizocheza Nyumbani na kuikaribia Arsenal ambao wapo kileleni na pia kuishusha Liverpool iliyokuwa Nafasi ya Pili na kuitupa Nafasi ya 4. 

Wakati Liverpool hii leo ikichapwa Bao 3-1 na Hull City, Chelsea ilishinda kwake Stamford Bridge kwa kutoka nyuma kwa Bao 1-0 hadi Haftaimu na kuifunga Southampton Bao 3-1.
Bao za Chelsea zilifungwa na Gary Cahill, John Terry na Demba Ba, alieingizwa Kipindi cha Pili.
Bao la Southampton, lililofungwa katika Dakika ya Kwanza tu, lilipachikwa na Rodriguez.
Huko Etihad, Bao la Negredo na mbili za Samir Nasri, ziliwapa Manchester City ushindi wa Bao 3-0 walipoichapa Swansea City.

Ushindi wa leo umeifanya Chelsea ikamate Nafasi ya Pili ikiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Arsenal na Nafasi ya Tatu imeshikwa na Man City walio Nafasi ya Tatu na wapo Pointi 2 nyuma ya Chelsea.
Jay Rodriguez ndie alieanza kuifunga Chelsea na kuipatia bao timu yakePongezi za aina yake hapa!!Wachezaji wa Chelsea hoi!John Terry kunani hapa!!Rodriguez akichuana na  Ivanovic wa Chelsea kushoto nyuma.,.Oscar kiatu kilimpitia ...chini akijiuguzaMajanga!!Victor Wanyama na Juan Mata wakigombea kutwaa mpira hapa!Branislav akigonga mpira kwa kichwaDemba Ba akitupiaIvanovic na Cahillwakipongezana baada ya kupata baoCapten John Terry akifana 2-1Pamoja na kufunga bao hilo la pili Jose Mourinho bado alikuwa anahitaja mabao mengine zaidiDemba Ba akisindikiza mpira nyavuni na kufunga bao la ushindi dhidi ya Southampton usiku huuFuraha ya Ushindi: Ramires, Demba Ba na wakiponezana na kupeana tano!!

No comments:

Post a Comment