Pages

Monday, December 30, 2013

CHEKA ATETEA KIPIGO CHAKE URUSI

BONDIA Francis Cheka amejitokeza hadharani na kusema kuwa kupigwa kwake ni sehemu ya mchezo na yeye ni kama mabondia wengine wanavyopigwa

Akizungumza jijini juzi, Cheka alimshangaa promota J. Msangi kwa kuongea kupigwa kwake na kusema mkanda alioupoteza hakiwa nao huku hana pesa  mfukoni haina maana yoyote.

“Unakaa na mkanda ili uonekana una mkanda tu wakati mfukoni huna pesa na una mahitaji na majukumu yanayohitaji pesa huo mkanda unaweza kutatua shida zako?, alihoji Cheka.

Pia alisema kuanzia acheze pambano na Phil Wiliams wa Marekani na kutwaa huo mkanda ambao pesa yake ilikuwa ni milioni 3.5 tu hajawahi kucheza pambano linguine zaidi ya ili la Russia alilopigwa huku akisema ngumi ndio ajira yake.

Cheka ambaye hivi karibuni alichezea kichapo cha KO kutoka kwa Fedor Chudinov wa Russia na kusababisha kuvuliwa  mkanda wa WBF alioupata baada ya kumpiga bondia Phil Williams wa Marekani kwa pointi jijini Dar es Salaam.

Mpambano huo ulifanyika nchini Russia katika Ukumbi wa Dynamo Palace of Sports in Krylatskoye ni wa kwanza kuchapwa baada ya kutawazwa kuwa bingwa wa WBF, mkanda ambao anaushikilia  lakini kutokana na sheria za WBF ukipigwa kwa KO kwenye mpambano wa kirafiki unapoteza mkanda huo.

Kwa kipigo hicho Cheka ameporomoka kwenye viwango vya ubora vya WBF toka nafasi ya 20 hadi 48 na inamlazimu kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kuwa anaomba kugombea mkanda wa WBF kabla ya Januari mwakani.



No comments:

Post a Comment