Pages

Wednesday, November 20, 2013

WAREMBO WANNE WA TOP MODEL WASHINDWA KUJIUNGA NA KAMBI


Wakuu wa Vyombo vya Habari
TANZANIA.
                                                         

Kambi ya Tanzania Top Models iliyoanza 7.11.2013 katika Hotel ya JB Belmont inaendelea vizuri ikiwashirikisha washiriki 16 badala ya 20 waliokuwa wamechaguliwa kujiunga na kambi hii. Wasichana walioshindwa kujiunga na kambi kwa sababu mbali mbali hasa kutokana na shule au kukataliwa na wazazi ni Esther Albert wa Dar es salaam, Jackline Kimambo wa Dodoma, Neema Selei wa Arusha na Esther Frederick wa Moshi. “Tunamshukuru Mungu leo ni siku ya 14 wasichana wakiwa kambini” na mambo yakiendelea vizuri ingawa kumekuwepo na changamoto kadhaa kama kuugua kwa baadhi ya Models na mapungufu ya vitu vidogo vidogo kutokana na kutokuwepo wadhamini wa kutosheleza mahitaji yote. Kambi yetu ilihama katika Hotel JB Belmont na kuhamia hapa tulipo kwenye Hotel Tamal siku ya Jumatatu 18.11.2013 na tunaendelea vizuri na mazoezi yetu, washiriki wetu wakiwa katika hali nzuri na wenye hamasa ya kushindana hapo ifikapo 7.12.2013.

Mashindano yetu ambayo yatakuwa sehemu ya shamrashamra za kusheherekea miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara, yatahusisha washiriki kuvaa na kuonyesha mavazi ya aina nne. Mavazi hayo yatakuwa ni Vazi la kitanzania(Tanzanian Dress), vazi la kubalizi (Cocktail Dress), Vazi la kiofisi(Office Dress) na Vazi la Jioni Evening Dress. Pamoja na Wanamitindo hawa kushindana katika mavazi, pia watashindana katika vipaji hadi tupate mshindi ambaye atatuwakilisha katika mashindano ya Top Model of the World yatakayo fanyika mwezi wa March 2014. Tunaendelea kujiandaa na shindano hili kwa washiriki kufanya mazoezi ya kutosha na kwa waandaji kuendelea kutafuta wadhamini na kutimiza wajibu wetu ili shindano letu liwe zuri na la kuvutia. Mazoezi yanayoendelea kwenye kambi yanaendeshwa na waalim sita. Zakia Twahir anafundisha kutembea (catwalk), Badspencer anafundisha na kuendeleza vipaji vya uchezaji wa muziki wa dance, Wanne Salim anafundisha na kuendeleza vipaji vya uchezaji wa ngoma na utamaduni, Dokta Cheni na Shuzi wanafundisha na kuendeleza vipaji vya kuigiza, ambapo ….. anafundisha na kuiendeleza vipaji vya kuimba.

Ni vyema tutumie nafasi hii leo kuzindua upigaji wa kura kwa washiriki wetu. Tunaomba wananchi waanze kufuatilia shughuli za washiriki leo usiku katika vituo vya Luninga vya Clouds TV na Tumaini TV ili waone kinachoendelea kwenye kambi na kupiga kura kwa mshiriki anaye kuvutia. Tunahimiza wananchi kupiga kura mara nyingi iwezekanavyo ili kumfanya mshiriki anayependwa na kupata kura nyingi aweze kushinda. Unachotakiwa kufanya wakati wa kupiga kura ni kutuma ujumbe kwa simu ya mkononi kwenda kwenye Namba 15564 ukiandika TM(unaacha nafasi) halafu jina la mshiriki unayempenda. Mfano unaandika “TM Jackline” na kutuma kwenda 15564. Majina ya Models wanaoshiriki na ambao wanaomba kura ni
·         AMMARA          . DARLINE         . EVE                    . GAUDENCIA
·         IRYNA                 . LORRAINE      . MATUREGE   . MIRACLE
·         NAIMA                                . NEMIC              . NILER                                . NURU
·         RETTY                                . GLADYS           . TINA                  . ZULPHER                       
Tunaomba wananchi watuunge mkono kwa kuendelea kupiga kura na kufanya mchuano wa kumtafuta Tanzania Top Model kuwa wa mafanikio na wenye tija. Mshiriki atakaye pata kura nyingi atajinyakulia Taji la Princess of Tanzania na kupata alama nyingi zitakazo mwezesha kushinda na kuwa Tanzania Top Model. Mataji mengine yatatolewa kwa Mwanamitindo atakaye pendeza zaidi katika vazi la kitanzania(best in Tanzanian Dress) pamoja na Tuzo kwa Mwanamitindo mwenye muonekano mzuri kwenye picha(Photogenic award). Mbunifu wa mavazi atakayekuwa amemvalisha Mshiriki atakayeshinda katika vazi la Kitanzania atapewa Tuzo kama Mbunifu bora wa vazi la kitanzania kwa mwaka 2013.

Ili kufanikisha shindano hili, tunao washirika ambao wako bega kwa bega na Kampuni yetu ya Tanzania Top Model Agency Limited,tunawashukuru sana.
1.    Data vision International - Mshirika wetu katika teknologia(Technology Ptner)
2.    Haakneel Production – Mshirika wetu kwenye uzalishaji (Production Partner)
3.    Giraffe Ocean View Hotel – Mshirika wetu kwenye Ukarimu (Hospitality Ptner)
4.    Clouds Media Group – Mshirika wetu wa Utangazaji.(Media Partner)
Pia tunao wadhamini mbalimbali ambao wametusaidia na wako tayari kufanikisha shindano hili. Tunawashukuru sana JB Belmont Hotel, For you Boutique, Shear Illusion, NSSF, Tamal Hotel, Screen Masters, TV Tumaini, Man Magazine, Fabak Fashion, TV Africa na Rio Gymn. Nafasi za kudhamini bado zipo na tunatoa mwito kwa wale wenye maono ya baadaye wajitokeze waje kutudhamini sasa ili tuweze kukua pamoja.
Tunashukuru vyombo vya habari vyote na hasa nyinyi mlioko hapa ambao mmekuwa mkifanya shindano la Tanzania Top Model kuwa katika masikio ya watanzania wengi na kulifanya liwe maarufu sana tangu kuzinduliwa kwake kinyume na tulivyotarajia.
Asanteni.



Jackson M.Kalikumtima
Mwenyekiti Mtendaji
Tanzania Top Model Agency Ltd


   20.11.2013

No comments:

Post a Comment