Pages

Friday, November 29, 2013

TANZANIA YAKAMATA NAFASI YA 124, PORTUGAL NA BRAZIL NDANI YA "TOP 10" SPAIN BADO KINARA

Wababe wa Dunia Spain, bado wanashikilia Nambari Wani katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Belgium na England zikiporomoka toka 10 Bora na Nafasi zao kuchukuliwa na Portugal na Brazil na Tanzania kupanda Nafasi 5 na kukamata Nafasi ya 124.
Kwa Nchi za Afrika, Ivory Coast ndio ipo juu kabisa na ipo Nafasi ya 17 ikibaki Nafasi yake ile ile na kufuatiwa na Ghana ambayo iko Nafasi ya 24.
Katika Nchi 20 Bora, ni Ukraine pekee ambayo haikutinga Fainali za Kombe la Dunia za huko Brazil zitakazochezwa Mwezi Juni Mwakani.
Listi nyingine itatoka Desemba 19.

NCHI 20 BORA:
1        Spain
2        Germany
3        Argentina
4        Colombia
5        Portugal
6        Uruguay
7        Italy
8        Switzerland
9        Netherlands
10      Brazil
11      Belgium
12      Greece
13      England
14      USA
15      Chile
16      Croatia
17      Côte d'Ivoire
18      Ukraine
19      France
20      Mexico

No comments:

Post a Comment