Pages

Friday, November 22, 2013

RONALDO HUENDA AKASHINDWA BALLON D'OR KAMA FIFA WAKIONGEZA MUDA WA KUPIGA KURA

Cristiano Ronaldo ameonekana kuelekea kuwamshindi wa tuzo FIFA ya Ballon d'Or na kumshinda mpinzani wake mkubwa Lionel Messi wakati huu ambapo kuna maamuzi ya kushtusha ya kuongeza muda wa kuendelea kupiga kura.
Hata hivyo imefahamika kuwa Ronaldo, ambaye ameendeleza kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda baada ya kufunga mabao matatu peke yake katika mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia (World Cup play-off) dhidi ya Sweden Jumanne usiku sasa anaonekana huenda akanyakua tuzo hiyo mjini Zurich Januari 13 ikiwa ni kama majibu ya dharau iliyoonyeshwa kwake na Rais wa FIFA Sepp Blatter.
Kiongozi huyo wa juu wa FIFA alidai kuwa nyota huyo wa Real Madrid anatumia muda mwingi kuhangaika na kutengeneza nywele zake pale alipoulizwa juu ya anavyolinganisha ubora wa mchezaji huyo na Messi, licha ya kwamba bosi huyo wa FIFA baadaye aliomba radhi.

Matchwinner: Cristiano Ronaldo netted a hat-trick against Sweden to secure Portugal's passage to Brazil
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya hat-trick dhidi ya Sweden na kukata tiketi ya Ureno kwenye kombe la dunia nchini Brazil
Franck Ribery
Lionel Messi

Wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo ni mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi (kushoto juu) ambaye mpaka sasa ameshashinda tuzo hiyo mara nne na Franck Ribery (kulia juu) ambaye anadhaniwa huenda akashinda kufuatia mafanikio na klabu ya Ujerumani ya Munich kufuatia kushinda mataji matatu msimu uliopita.

WHO CAN VOTE FOR THE GONG?

Kamati ya utendaji ya FIFA na kundi la wataalamu kutoka Ufaransa walipendekeza majian 23 ya washindani wa tuzo hiyo Oktoba 29. 
Mshindi ataamuliwa na makundi matatu ya wapiga kura. Kundi la kwanza ni la makocha na kundi la pili ni manahodha wa timu za taifa na kundi la tatu ni kupitia wanahabari.
Sheria inakataza wachezaji kupigiana kura. 
Ronaldo aliibuka shujaa huko Stockholm Jumanne na kuipelekea Ureno Brazil na Zlatan Ibrahimovic akiwa na kikosi kizima cha Sweden wakishindwa kufanya hivyo.

Magoli matatu ya Ronaldo, maarufu kama hat-trick katika klabu yake ya Real Madrid na hat- trick nyingine akiisaidia timu dhidi ya Sweden inatengeneza nafasi kuwa pana ya kushinda tuzo ya pili ya Ballon d'Or mwezi January.
Fallen hero: Zlatan Ibrahimovic's two goals were not enough to see off the threat of Ronaldo and Portugal
Mabao mawili ya Zlatan Ibrahimovic hayakutosha kumzuia Ronaldo na Ureno yake kutokwenda Brazil.

THE FULL 23-MAN LIST

Gareth Bale (Wales/Real Madrid) Edinson Cavani (Uruguay/PSG) Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid) Radamel Falcao (Colombia/Monaco) Eden Hazard (Belgium/Chelsea) Zlatan Ibrahimovic (Sweden/PSG) Andres Iniesta (Spain/Barcelona) Philipp Lahm (Germany/Bayern Munich) Robert Lewandowski (Poland/Dortmund) Lionel Messi (Argentina/Barcelona) Thomas Muller (Germany/Bayern Munich) Manuel Neuer (Germany/Bayern Munich) Neymar (Brazil/Barcelona) Mesut Ozil (Germany/Arsenal) Andrea Pirlo (Italy/Juventus) Franck Ribery (France/Bayern Munich) Arjen Robben (Holland/Bayern Munich) Bastian Schweinsteiger (Germany/Bayern Munich) Luis Suarez (Uruguay/Liverpool) Thiago Silva (Brazil/PSG) Yaya Toure (Ivory Coast/Manchester City) Robin van Persie (Holland/Manchester United) Xavi (Spain/Barcelona)
 
Katika hatua nyingine, Thiago Silva hatakuwa na uwezo wa kumpigia Neymar kwakuwa ni mchezaji anayetoka naye katika taufa moja la Brazil kama sheria inavyokataza.
Mlinzi huyo wa kati wa Paris Saint-Germain alinekana kufurahia hapo kabla juu ya kutaka kumpigia kura countryman Neymar.

No comments:

Post a Comment