Pages

Tuesday, November 19, 2013

QATAR MASHAKANI KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022 KUTOKANA NA UNYANYASAJI WA WAGENI

Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu – Amnesty International limeshutumu “kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa wafanyakazi wa ujenzi nchini Qatar, kwenye ripoti yake ya hivi punde.

Amnesty Internationa imeitaka Qatar kuitumia fursa ya kuandaa dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2022 kwa kuonyesha kuwa imejitolea kulinda haki za binaadamu. Ripoti ya Amnesty International inasema wafanyakazi wa kigeni wanaishi kama “wanyama“, neno ambalo shirika hilo limesema watafiti wake walimsikia mkurugenzi mmoja wa kampuni ya ujenzi akilitumia kuwaelezea wafanyakazi hao.
 
Salil Shetty ni Katibu Mkuu wa Amnesty International na anasema "Kitu kimoja ambacho tunaamini kinapaswa kutatuliwa haraka ni mfumo wa kutoa vibali vya kuondoka. Tunadhani hilo linastahili kushughulikiwa haraka. Matatizo ya ukiukaji wa haki za binaadamu kuhusiana na wafanyakazi wa kigeni nchini Qatar ni makubwa mno. Yamesambaa kote. Siyo matukio machache tu".
Serikali ya Qatar inapinga madai hayo kuwa inawanyanyasa wafanyakazi wa kigeni, ikisema itayaijumuisha ripoti hiyo katika uchunguzi ambao tayari ilianzisha. Nasser 
ya ya afya na viwango duni vya usalama

No comments:

Post a Comment