Angetile Hosea (kushoto) akiwa katika moja ya mkutano na waandishi wa habari na aliyekuwa rais wa shirikisho la soka nchini (TFF), Leodegar Tenga |
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Angetile Hosia amepewa likizo ya mwezi mmoja NA nafasi yake itakuwa inakaimiwa na Ofisa Habari, Boniface Wambura.
Hatua hii imetokana na agenda iliyotolewa na Rais mpya wa Shirikisho hilo kwenye kikao cha kamati ya Utendaji iliyokaa jana kwenye hotel ya Courty Yard jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhiwa ofisi.
Angetile ajira yake kwenye shirikisho hilo ilikuwa inafikia mwisho Desemba 3, mwaka huu kufuatia taarifa iliyotolewa na Tenga wakati akikabidhi ofisi
Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati
ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama
shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika
utekelezaji wa majukumu yake.
No comments:
Post a Comment